HII NDIO FIRST ELEVEN YA MAJERUHI WATAKAOKOSA BRAZIL - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Sunday, May 25, 2014

HII NDIO FIRST ELEVEN YA MAJERUHI WATAKAOKOSA BRAZIL

Na Bakari Ally
Simu: 0684000544

Tokeo la picha la WORLD CUP 2014
Siku chache zimebakiwa kuelekea nchini brazil kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia  kuna wachezaji ambao watakosa kwa ajili ya majeruhi na wengine kukosa nafasi ya kuitwa na timu zao za taifa.
Ifuatayo ni first elven ya majeruhi watakaokosa brazil huku 4-3-3 au 4-2-3-1 watatumia

1.VICTOR VALDES (HISPANIA)
Huyu ni kipa namba moja wa timu ya barcelona pia ni nafasi ya pili kwenye timu ya taifa nyuma ya Casillas.
Anasumbuliwa na Ligament tangu mwenzi wa tatu na nafasi yake amechukua David Gea

2.MAKOTO HASEBE (JAPAN)
Huyu ni kiungo mkabaji pia anaweza kucheza kama full back ya kulia anachezea timu ya Nurnberg ya ujerumani pia ni nahodha wa timu ya taifa ya japan.mwezi wa pili alifanyiwa upasuaji mara mbili katika mguu wake.

3.JETRO WILLEMS (UHOLANZI)
Ni mtoto wa miaka 20 ambaye anacheza namba 3 kwenye timu ya PSV na tulimuona kwenye michuano ya Euro mwaka 2012, nae anasumbuliwa na mguu.

4.SILVIO (URENO)
moja ya mabeki wazuri wa ureno lakini silvio ameumia tibia(mfupa mwembamba) na fibula (mfupa mkubwa) kwenye mguu wake kwenye mechi ya Europa ligi dhidi ya Az Alkmaar akimpiga mchezaji mwenzake baada ya mpira.

5.HOLGER BADSTUBER (UJERUMANI)
Beki wa munichen mara ya mwisho kucheza ilikuwa mwezi wa 11 mwaka 2012 anasumbuliwa na Cruciate ligament.

6.STUART HOLDEN (USA)
Japokuwa yupo timu ambayo sio kubwa bolton wonderz ila ndio nahodha wa marekani ila anasumbuliwa na mguu wake wa kushoto na kwa sasa yupo Shiefield wensday kwa mkopo kiungo mkabaji ndio nafasi yake.

7.THEO WALCOT (UINGEREZA)
Hakuna asiyemjua walcot uwezo wake wa kukimbia huku akipiga chenga mara ya mwisho kuonekana uwanjani ni mwezi wa kwanza mwaka huu kwenye mechi ya F.A dhidi ya spurz.

8.KEVIN STROOTMAN
(UHOLANZI)
mchezaji wa Roma akiwa anacheza kama kiungo wa kati pia na nyuma ya striker msimu uliopita man utd walitaka kumsajili lakini ikashindikana ameumia tangu mwezi wa tatu.

9.CHRISTIAN BENTEKE
(UBELGIJI)
Aliumia mwezi wa 10 na akikadiliwa atakuwa nje kwa miezi 6 au zaidi akarudi uwanjani mwezi wa nne lakini ameumia tena mwanzo wa mwezi huu.

10.JAY RODRIGUEZ (UINGEREZA)
Ni mshambuliaji wa southamptom nae anasumbuliwa na mguu tangu mwezi wa 4.

11.LUIS SUAREZ (URUGUAY)
Juzi jumatano akiwa mazoezini ndipo aliumia na jana amefanikiwa kufanyiwa upasuaji wa mguu wake,japokuwa shirikisho la soka la uruguary wanasema suarez lazima acheze kwa kuwa atakuwa amepona.

FORGIVE ME

No comments:

Post a Comment

Pages