NAKWENDAA MILAN: THE DEMISE OF MILLAN CITY, SO SAD - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Saturday, December 16, 2017

NAKWENDAA MILAN: THE DEMISE OF MILLAN CITY, SO SAD

 Na: Bakari Ally
Simu: 0659767121

Baada ya kukaa  mdogo wangu yuko busy anachezea Play station game, huku mie nikiwa napitia kitabu cha "Going within" kimeandikwa na shirley maclaine, ndipo nikaulizwa swali kuwa utajisikiaje endepo Ac Millan ikitwaa ubingwa wa Italy msimu huu, kwa tabasamu nanyanyuka namwambia "Nitazima play station, alafu nifanye assignment za chuoni", wakati huyo baada ya kujibu ndipo nikiwa naelekea gengeni mara moja kuchukua vocha naona picha ya Inzaghi imebandikwa kwenye gari.
Tokeo la picha la inzaghi vs kaka
Pichani ni Pipo Inzaghi kulia na Ricardo kaka kushoto


Unajua nimekumbuka nini, ilikuwa mei 23 mwaka 2007 ambapo muitaliano huyo akiifungia Ac millan magoli mawili dhidi ya FC Liverpool katika uwanja wa Olympic Stadium, huku mji wa Anthens Ugiriki kulikuwa na watu takribani 60,000. Mara naitwa kaka wewe chenji yako baada hii nilikuwa natoka gengeni hapo ndipo, Narudisha kumbukumbu kwa Ricardo Izecson dos Santos Leite wengi tulikuwa tunamuita kama Ricardo kaka, sikuhiyo hapo Anthens ndie alitoa pasi ya goli la pili mnamo dk 82, pia tunamkumbuka kaka amewahi kuwa mchezaji bora wa dunia.

Niko narudi nyumbani naiona jezi ya Diego Milito ndipo chozi linakaribia kunitoka najikaza nafika nyumbani nachukua simu naweka bando naingia you tube naangalia marudio ya fainali ya uefa 2010 ndipo naona Diego Millito huku jose Mourinho "The special one" akiwa kocha wa Inter Millan wananyanyua makapwa wakiwa na taji la uefa la mbele ya Bayern Munich, Diego Millito anafunga goli mbili?, yote tisa Ribery na Roben walikuwa wamoto, lakini Inter walitwaa taji hilo.
Tokeo la picha la jezi ya diego millito
pichani ni Diego Millito Inter Millani


Nakuja kuandika hii makala kwa sababu, Jiji la Millan ambapo lilitawaliwa na miamba Inter na Ac Millan zote hizo zimepotea kwanye ulimwengu wa soka, Wakati Ac Millan anachukua ubingwa mwaka 2007 lilikuwa ni taji la saba huku ikiwa ni timu ya pili iliotwaa mara nyingi taji hilo, Real Madrid ilikuwa imetwaa mara tisa lakini hayo yote sawa na FC Barcelona walikuwa wametwaa mara mbili tu(walikuwa wamewazidi Barca mataji matano)
Mara ya mwisho kwa Ac millan kutwaa taji la Serie A ni 2010/11, Coppa Italia 2002/03, Supercoppa Italiana 2011, Uefa 2007. Lakini mpaka sasa hivi Real Madrid imetwaa Uefa mara 12 na barcelona mara tano, kwenye Ligi anamaliza nafasi ya 7,8,10.

Tokeo la picha la burlusconi vs Thohir
Mmiliki wa Inter Millan Erick Thohir
Wakati Inter wanatwaa 2010 taji la UEFA ni wazi kuwa ilikuwa na timu ya wazee kuanzia Golini mpaka washambuliaji, Julio Cesar, Maicon, Chivu, Zanneti, Cambiasso, Sneijder wesley, Eto'o, Millito na Goran Pandev wote walikuwa na Umri mkubwa, lakini walikuwa na uwezo mkubwa na wengine sio wazee lakini walitumika sana.


Timu hizi zilianza kupotea mwaka 2005 kutokana na kashfa ya upangaji matokeo ambapo timu ya Juventus ilishushwa daraja, taratibu ligi ilianza kupotea na Ac Millan ilizidi kupotea baadaa ya kuyumba kwa uchumi timu ilishindwa kutengeneza vijana na kusajili wachezaji wenye adhi ya timu huku wachezaji wake wakitundika daruga soka la ushindani na wengine kwenda timu nyingine Kaka uliuzwa 2009 kwenda Real, Pirlo aliuzwa 2011 kwenda Juventus pia Etoo aliondoka, Balloteli aliuzwa Man city, Pandev(Inter) aliondoka 2012 na Philipe Coutinho alienda Liverpool 2013.

Timu hizo zilijitahidi kurudi kwenye chati kwa kutenga donge nono la usajili, mwaka 2009 Massimo Moratti alikuwa na £350 millioni kwa ajili ya usajili lakini timu mpaka kufikia 2011 ikaletwa Financial Fair play Inter millan wakaacha kusajili wachezaji ghali, mwaka 2013 Massimo alikubali kuuza 70% za hisa zake kwa Muindonesia Erick Thohir.

Mwaka 2014 tulishuhudia timu ya Inter ikisajili watu kama Fred Gurian, Mateo Kovacic, Hernanes, Xhaden Shaqir lakini juu ya hayo yote timu ilishindwa kumaliza katika nafasi tatu za juu huku wakimaliza nafasi ya nne na waliachwa jumla ya alama  24 na mabingwa Juventus.

Ac Millan ambazo ilikuwa chini ya Silvio Berlusconi ambae alikuwa waziri mkuu imejitahidi kurudi kwenye hali yake lakini imeshindwa imetumia njia ya kurudisha wachezaji wake wa zamani au kuleta wenye mafanikio kama kumrudisha Kaka, Ronaldinho, David Beckham, Michael Essien na Fernando Torres kwa wakati tofauti, Lakini timu imekosa kurudi kwenye hali ya zamani. Mwaka 2015 walitumia £80 millioni kusajili wachezaji watano akiwemo 
carlos Bacca na timu ilimaliza katika nafasi ya saba wakati msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya 10. Mpaka sasa Millan ina wachezaji kama Donnarumma, Abate, Antonelli, alex, Honda, Montolivo, bacca nk.
Tokeo la picha la millan squad 2017
Kikosi cha Ac Millan, miaka mitano imepita sasa

Lakini pia makocha tofauti tofauti wamepita timu hiyo kuanzia mwaka 2014  mpaka 2017, Ac Millan Massimo Allegri alikuwepo 2014, lakini baadae akafukuzwa baada ya kufanya vibaya akaja Clerence Seedorf nae akapigwa chini baadae akaja Filipo Pipo Inzaghi na sasa wamemteua Gennaro Gattuso awe kocha wa timu hiyo, pia alipita Sinisa Mihajlovic ambapo alifukuzwa mwaka 2016 na Cristian Brocch
Huku kwa upande wa Inter Millan wamepita makocha kama Raphael Benitez, Leornado, Gian Gasperin, Claudio Ranier, Andrea Stramaccioni na Water Mazzari. Kikosi cha Inter kwa sasa ni wakina Handonovic, Miranda,nagatomo, joao Mario, Valero, Perisic, candreva, Icardi, Eder nk nguvu yake sio sawa na wakina Millito waliotwaa mataji matatu (Treble) 2010 chini ya Mourinho.

Mwisho wake sioni kabisa uelewekeo mzuri wa timu hizo hakika Ac Millan nimeimisi enzi zile za Paulo Maldini, Andrea Pirlo, Gennaro Gattuso, Massimo Ambrosin, Mark van Bommel, Alesandro Nesta, Kaka na Seedorf, kwa upande wa Inter nimemisi kile kikosi cha Mourinho 2010 watu kama Sneijder, Pandev, Etoo, Countinho, Balloteli lakini kwa sasa nimeona hakuna dalili ya kurudi zile timu za Millan nabaki nasikitika na kuamua kuandaa safari ya kuliacha jiji la Millan kifikra niendelee na Majukumu ya kujenga taifa.




No comments:

Post a Comment

Pages