Israel ilivyowaduwaza wanajeshi wa Idd Amin katika Operation Thunderbolt (Entebe 1976) - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Saturday, June 9, 2018

Israel ilivyowaduwaza wanajeshi wa Idd Amin katika Operation Thunderbolt (Entebe 1976)

Story na:Bakari Jr
Simu:0659767121

Ilikuwa mwaka 1976/27/Juni, Ndege ya Ufaransa A300 Airbus iliyokuwa ikitokea Tel Aviv nchini Israel huku ikielekea Mjini Paris jijini Ufaransa ikapitia ugiriki Athens ilitekwa na magaidi wawili wa Kipalestina kutoka kikundi cha PFLP-EO chini ya kiongozi wao Wadie Haddad na magaidi wawili wa Ujerumani kutoka kwenye kikosi cha Revolutionary Cellls, ikiwa na abiria 248 wengi wakiwa ni waisrael.

Watekaji hao wa kipalestina walisema lengo lao ni waachie watu wao arobaini waliokamatwa katika nchi ya Israel pia wanajeshi wao 13 waliokuwa wamefungwa katika nchi nne tofauti ili waweze kuwaachia mateka hao.

Ndege hiyo ilibadirishwa mwelekeo kutoka Anthens mpaka  Benghazi, na kupelekwa nchini Uganda uwanja wa ndege wa Entebbe, na Amin akaweka walinzi wa kuilinda,
Baada ya ndege kufika katika uwanja wa Entebe nchini uganda Iddi Amini alikuwa amewakaribisha na kuwekea ulinzi ndege hiyo, Siku ya tarehe 29-Juni watekaji wakaanza kuwatenga wale mateka wa kwenye ndege Mayahudi (waisraeli) na wasiokuwa Mayahudi na kuwaweka katika Vyumba tofauti.

Baada ya siku mbili ina maana tarehe 30-Juni mateka wote ambao sio mayahudi waliachiliwa na kupandishwa ndege ambayo iliruka mpaka Paris nchini Ufaransa, Huku mateka 94 wa kiisraeli wakishikiliwa na mateka wengune 12 wa Air France Crew, Huku wakiwatisha kuwa watawaua. Moja ya mateka hao alipelekwa hospitali kupata matibabu. Lakini magaidi wakasema kuwa mwisho ni tarehe 1 Julai vinginevyo wanachinja ama kuua mateka hao.

SASA OPERESHENI YA KUKOMBOA MATEKA

HUU NDIO MCHORO WA OPERESHENI NZIMA YA ENTEBE

Baada ya habari kuwafikia Israel waliomba baraza la usalama la usafiri wa anga usijisumbue kuingilia suala ilo bali watamaliza wenyewe, Kiongozi wa zamani wa kikosi cha usalama cha Israel  bwana Baruch "Burka" Bar-Lev alikuwa na uhusiano na Iddi Amini ambapo alimpigia simu mara kadhaa ili kufanya diplomatic solution.
Ilipofika tarehe moja mapema tu Cabinet ya Israel iliongea na watekaji kuwa waongeze deadline mpaka tarehe 4 Julai.

Sasa kufikia tarehe 3 Julai muda ni saa 12:30 jioni Cabinet ya Israel ikapitisha Misheni ya kuwakomboa mateka, Misheni hiyo iliandaliwa na Major General Yekutiel "Kuti" Adam huku bwana Brig. Gen. Dan Shomron. Shomron aliteuliwa kuwa Operesheni Komando.

Misheni ilikuwa kwa kutafiti mambo yafuatayo
1. Uwanja na muundo wa uwamja wa Entebbe ulivyo,
2. Gari la Idd Amini muundo wake, ulivyo na aina yake,
3. Wakagundua umbali wa kutoka uwanja ulipo mpaka makao ya jeshi yalipo,
4. Wakataka kujua mateka walipotunzwa,
 
Ikumbukwe Ehud olmet ndie aliyepiga picha za mwanzo kwa ndege ya kibinafsi uwanja wa entebe na kuzituma Israel kwaajili ya maandalizi ya operation .

Baada ya kugundua hayo walifanya yafuatayo
Wakatafta gari kama la Idd amin na rangi ilivyo na plate number ya kufoji,
Wakatafuta ndege tatu za kivita,
Wakaandaa wanajeshi kadhaa na makomandoo 35 wakiwa na mavazi ya wanajeshi ya uganda ,

Majira ya saa 5 usiku Wakaanza safari mpaka Entebe ndege ya kwanza ilitangulia iliyokuwa na magari natatu ya kufanana na convoy ya Amin,
Ndege zao za kivita ilibidi ziende juu meter 30 kuzuia detection, maana ikienda juu ya hapo itakuwa detected na radar za nchi kama Egyptian, Sudanese, na Saudi Arabian kwa sababu ilipita kupitia bahari nyekundu. Baadae ndege ilipita maeneo ya kusini mwa Djibout, Nairobi, Somalia na baadae Ziwa Victoria, hiyo ni ndege ya kwanza.
WANAJESHI WA ISRAEL

Ndege nyingine mbili zilichelewa kufika, moja ilibeba madawa na kutua Jommo Kenyatta International Airpot, ndege nyingine ilikuwa imefika uwanja wa Entebe huku akiwa mkuu wa kikosi ndani yake General Yekutiel Adam.

Baada ya kufika magari matatu yakatoka kwenye ndege na kupita V.I.P japo gari la kwanza lilishtukiwa ambapo kulikuwa na mtaalamu  General Yekutiel Adam ilibidi wajeshi wa Israel watumie silent pistol kuwanyamazisha.

Wakapita vema na njian kwingine hawakupata tatizo maana ilikuwa ni kama masafara wa Rais ,

Baada ya kufika hapo vita ilipiganwa dakika 53 tu na kuwakomboa mateka

Kikosi maalumu kiliingia uwanja wa ndege na na kuelekea katika jengo kuu kabisa la uwanja huo ambapo mateka walihifadhiwa na baadae wakaongeza kupitia kipaza sauti kuwa "Stay down! Stay down! We are Israeli soldiers,"
katika misheni hiyo kijana wa kifaransa mwenye miaka 19 alipigwa risasi na Makomando wa kiisraeli baada ya kumfikiria vibaya labda ni mtekaji, huku mwingine alipigwa risasi na Mtekaji, baadae bwana Pasco Cohen alikuwa na miaka 52 alijeruhiwa vibaya sana.

Walikufa wanajeshi 139 wa Uganda, huku wakiwauwa matekaji wote na  Kwa upande wa Israel alikufa mwanajeshi mmoja na Muhim Jonathan Netanyahu kaka wa waziri mkuu wa sasa Benjamin Netanyahu.

Operation ikaisha , wakapandisha mateka na kurudi Tel Aviv , Kumbe kuna mama mmoja alisahaulika wa Israel, kwenye chumba maalumu cha hospital, kwa hasira Idd Amin alimuua kwa kumchinja na kuondoa moyo wake.

Pia karibu makomandoo wengi walioshiriki operation thunderbolt wengi walikuwa majenerali wa jeshi baadae yani Rav alafu au prime ministers na wakuu wa vitengo mbalimbali mfano Ehud olmet, Ehud barak, na Benjamin netanyahu, Hawa wote walikuwa mawaziri wakuu baadae lakini wote walishiriki operation hatari sana ya thunderbolt.

VIDEO FUPI KWA LOTE LA SIKU HIYO



No comments:

Post a Comment

Pages