GOAL MORNING: Ross Barkley's solo strike against Newcastle - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Saturday, September 1, 2018

GOAL MORNING: Ross Barkley's solo strike against Newcastle

Image result for ross barkley everton

Ross Barkley ni moja ya vijana ambao wamejaliwa kipaji cha mpira huku akiwa na uwezo wa kumiliki mpira, kupiga chenga, kufunga pia kukaa na mpira muda mrefu, Lakini leo hii kwenye goal morning nimekuletea moja ya goli lake alilofunga akiwa na Everton dhidi ya Newcastle katika dimba la St James Park.

Image result for ross barkley everton vs newcastle

Goli hili ni goli ambalo amefunga kwa juhudi zake mwenyewe maarufu kama Solo Goal, Wakati Everton wakilinda mpira wa kona katika goli lao, baada ya kuokoa mpira huo na kichwa ukafika katika kifua cha Gerard Deulofeu, ndipo akamuekea Ross Barkley umbali wa yadi 70 uelekeo wa goli la upinzani, akawa anakimbia nao kwenda mbele huku wechazaji wenzake wenye mbio kama Lukaku wakiwa wamefika katika eneo hilo huku wakiomba mpira, Lakini Barkley akaingia nao katika eneo la penati akimuacha beki Fabio Collocini nyuma yake alafu kwa guu la kushoto akapiga mpira na kufunga goli.

http://worldsoccertalk.com/wp-content/uploads/2014/03/barkley.gif



No comments:

Post a Comment

Pages