Moja ya stori ambazo zimekuwa zikisimuliwa sana karne ya 21 ni kutokana na kijana ambaye aliishi katika karne ya 19 (1887-1910) katika nchi ya uingereza, Edward Mordake ambaye alizaliwa mnamo mwaka 1887 akiwa na sura mbili, moja ya kawaida na nyingine ipo kisogoni mwake.
Sura hiyo ilikuwa na msichana ambaye kama amevaa kinyago na ilikuwa inachukua sehemu ndogo ya kisogo chake, sura hiyo ilikuwa na macho, pua na mdomo na ilikuwa inaelezewa kama "Lovely as dream, hideous as a devil"
Sura ya Mordake ambayo ipo kisogoni mwake ilikuwa haiwezi kuona wala kuongea kwa sauti, isipokuwa ilikuwa inatabasamu pale alipokuwa na huzuni, na kulia wakati Mordake ana furaha.
Mordake alikuwa anaishi kwa upweke muda wote akiwa chumbani kwake, huku akiwa hapendi kutembelewa na watu na pia hata familia yake.
Mordake alisema kuwa sura hiyo ikifika usiku sura inamnong'oneza maneno ya kuzimu na kuipa jina sura hiyo kama "DEVIL TWIN," kiasi ambacho kilikuwa kinamfanya anakosa usingizi na kuuita, Mordake alikuwa anasema kuwa hakuna kitu ambacho atafanya na hili kuondoa hofu ya sura hiyo ya pili.
Mordake aliwaombia madaktari wamfanyieoperesheni ili kuiondoa sura hiyo "demon face" lakini ilishindikana kufanyika kwahivyo kutokana na ugumu, na kutokana na hili madaktari walisema kuwa deformity hiyo imetokana labda kwa kushindikana kwa kutokea mapacha.
Kutokana na sura hiyo ya pili ndio ilimfanya awe anawaza kujiua, siku moja Mordake alifanikiwa kupata sumu na kunywa akiwa na miaka 23, na sababu ya kujiua ilikuwa ni sura ya pili, na aliagiza familia kuwa asizikwe na sura hiyo, kwahiyo sura hiyo ilitakiwa kuharibiwa kwa kuwa alisema itakuwa inaendelea kumnong'oneza akiwa kaburini.
KWANINI STORY HII HAIAMINIKI?
Katika karne ya kumi na tisa ni kweli watu wengi walikuwa wanazaliwa na body deformities lakini hadithi hii imekuwa ngumu kukubalika kwa sababu ya kwanza kama ni kushindikana kuwa machapa ina maana Mordake alikuwa ni Mapacha waliogandana kisayansi mapacha waliogandana wanakuwa na jinsia moja, Pili hakuna mtu ambaye amewahi isikia sauti hiyo na sura ya nyuma, Tatu kukosekana kwa ushahidi.
No comments:
Post a Comment