Moja ya stori zilizotokea miaka ya 2014-2015 ni ya kijana wa kiarabu raia wa Uingereza ambaye alikuja kuwa tishio la dunia baaada ya kujiunga na kikundi cha ugaidi kinachojulikana kama Islamic State.
Kijana huyu alikuwa anajulikana kwa Jina la Jihad John, huku akiwa maarufu sana kwa kuonekana kwenye video akiwa na mask huku anachinja.
Ni Nani Huyu?
Kwa majina halisi ni Mohamedi Emwazi, alizaliwa mwaka 1988 katika nchi ya Kuwait, ambapo akiwa na miaka sita familia yake ilihamia Uingereza na kuishi magharib mwa London, alisoma primary shule ya St Mary Magdalene Church iliyopo uingereza na baadae kujiunga na Quintin Kynaston School.
Mwaka 2006 alianza chuo kikuu cha Westminster akichuka shahada ya sayansi katika mfumo wa mawasiliano pamoja na biashara(Bsc of Information System with Business Management) ambapo alimaliza kwa kupata lower second class with honors.
Maisha yake yalikuwaje?
Mohamedi Emwaz ni mtu ambaye alikuwa mpole, mwenye nidhamu na adabu kwa mujibu wa wazazi, wanafunzi na muajiri wake alithibitisha hilo.
Kwanini Jihad John na sio Emwaz?
Mohamedi Emwaz alikuwa anafahamika kama Jihad John ikiwa kama jina la utani, Jina la John lilitokana na kuwa katika kikosi chao cha uhalifu/uhuni kujiita "The Beatles" Band ya zamani ya muziki, kwahiyo Mohamedi Emwaz na wenzake walipeana majina kutoka kwa wasanii wa The Beatles na Emwaz kuita jina la John ikiwa na maana ya John Lennon wa kundi la The Beatles, Wakati majina mengine kama Jihad John. Jailer John na John the Beatles yaliundwa na waandishi wa habari.
Maisha baada ya kumaliza elimu
Baada ya kufanya mahafali mwaka 2009 katika chuo kikuu cha Wistminster, Mwezi Mei 2009 ripoti zinasema Jihad John na wenzake wawili walifika nchini tanzania na kutua katika uwanja wa Mwalimu Julius International Airport na kwa bahati nzuri polisi waliwazuia kuingia kwa kuwa walikuwa wamelewa sana na kuongea matusi, pia kwa taarifa ya zinasema aliruka na ndege mpaka Amesterdam(uholanzi) ambapo M15 anataka kwenda nchini Somalia kwa kundi la Al shabab.
Idadi ya watu aliowachinja
Haijulikani ni watu wangapi walikata vichwa na Jihad John lakini watu ambao walijulikana ambao ni maarufu pamoja na,Mwandishi James Foley ambaye video yake iliwekwa katika mtandao wa you tube mwaka 2014 mwezi agosti, video hiyo ilikuwa inamuonesha Jihad john akitumuambia Foley kuwa aseme uuchafu wa Marekani na aliposhindwa fanya hivyo Jihad John alikata kichwa, Pia mwezi wa tisa ilirushwa video ikionyeshwa muandishi wa marekani Steven Stoloff akikatwa kichwa na Jihad John.
Kundi kubwa la wanajeshi wa Syria walikata vichwa na Jihad John kwa live, kumbuka video za mwanzo zilikuwa akitaka kukata kichwa kamera inazimwa, sasa safari hii alionyesha live namna ambavyo anakata vichwa vya watu ambapo ilikisiwa si chini ya 12 au 18.
Kujulikana kwa Jihad John
Video zote zilikuwa zinaonyesha mtu mwenye kinyago usoni huku akiwa amevalia nguo nyeusi, huku akiacha macho na viatu sio vyeusi, video zote alikuwa anaonekana amebeba bunduki akiweka begani, rangi ya ngozi ndipo maafisa wa upelelezi walijua kuwa ni muafrika au ni tu wa Asia, pia alijulikana kutokana na kimo chake, muonekano, na mishipa yake(Vein), sauti na nguo zake, Timu ya maofisa upelele ukiongozwa na Sir Peter Westmacott alisema kuwa uingereza itaweza mtambua mtu huyo kwa kutumia teknolojia ya Voice recognition.
Mkurugenzi wa FBI James Comey aliwaambia wandishi kuwa "Mtuhumiwa tumemfahamu wasifa wake na utaifa wake. Mpaka kufikia febuari 2015 jina la Jihad John lilijulikana kama ni Mohamedi Emwaz ndipo ndugu na jamaa wakaanza kutafuta.
Kifo cha Jihad John
Mwaka 2015, November 12 katika mji wa Raqqa nchini Syria shambulizi lililofanywa na ndege zakivita za kimarekani ambapo inasemekana kuwa Emwaz (Jihad John) alikuwa anatoka ndani ya nyumba a kuingia kwenye gari ndipo likapigwa hilo shambulio.
Mwaka 2016 januari 19 kikundi cha Islamic state kilithibitisha kuwa Jihad John amefariki katika shambulio lililofanyika Raqqa.
No comments:
Post a Comment