STAAJABIKA NA NA KESI HII YA MAUAJI YENYE UTATA ZAIDI. March 23 mwaka
1994 tabibu mkaguzi(medical examiner) anauchunguza mwili wa marehemu
Ronald Opus na kufikia maamuzi kua Ronald Opus alikufa kwa kupigwa
risasi kichwani, Hii inatokana na jeraha kubwa la risasi kichwani
alilokutwa nalo marehemu Ronald Opus...
Hapa ndipo tabibu mkaguzi pamoja
na vyombo vya usalama wanakubaliana kua wana muuaji mikononi mwao..
Mpaka kufikia hatua hio,uchunguzi uliofanyika awali na vyombo vya
usalama unabainisha kua marehemu Ronald Opus alijirusha kutoka kwenye
jengo la ghorofa kumi kwa lengo la kujiua, aliacha kikaratasi chenye
ujumbe mfupi kwenda kwa wazazi wake chenye maneno yafuatayo
"I'm sorry I
can't forgive you, I will be with God " (nisamehe, siwezi kuwasamehe,
ntakua na Mungu) Marehemu Ronald opus alijirusha kutoka ghorofa ya kumi
kwa lengo la kujiua,lakini wakati akishuka chini alipigwa risasi ya
kichwani(juu kwa juu kabla hajafika chini) hali iliyopelekea kusitisha
maisha yake papo kwa hapo Si marehemu Ronald wala aliyefyatua risasi
alikua akijua kua kwenye jengo lile kuliwekwa neti za usalama(safety
nets) kwa ajili ya kuwalinda waosha vioo wa jengo lile. Hizi neti za
usalama hua zinawekwa kabla hujafika chini kwenye majengo au madaraja
marefu ili ikitokea mtu akianguka basi aangukie kwenye hizi neti za
usalama na asipate madhara.
Mwili wa marehemu ulikutwa juu ya hizi neti
za usalama, kwa maana hio kilichomuua Ronald ni risasi aliyopigwa angani
na wala si kingine, isingekua risasi ile,dhamira yake ya kujiua
Isingetimia...
RISASI ILITOKA WAPI NA HUYU MUUAJI NI NANI?? Vyombo vya usalama
vinaingia kazini, wanafanya uchunguzi wa kina(vetting) kwenye jengo lile
lote na kubaini kua risasi iliyomuua Ronald Opus ilitoka kwenye chumba
kilichopo ghorofa la 9 la jengo lile, hii ni kutokana na kukutwa kwa
tundu la risasi katika moja ya madirisha ya chumba kile.
Chumba hiki
anaishi mzee wa makamo pamoja na mke wake, baada ya mahojiano inabainika
kua mzee yule alikua na ugomvi mkubwa na mke wake, hii ilipelekea mzee
yule kumshikia bunduki mke wake, mzee huyu alikua akitetemeka sana
kutokana na hasira hali iliyopelekea kutoweza kushika bunduki
vizuri,hivyo alivyofyatua risasi ilimkosa mke wake na kupita dirishani
ikampata Ronald aliyekua kwenye harakati zake za kujiua SHERIA
INASEMAJE??
Mtu ukiwa na lengo la kumuua mtu 'A' lakini katika jaribio
hilo kwa bahati mbaya ukamuua mtu 'B' basi unakua na hatia ya kumuua mtu
'B' Hapa wana usalama wakaona wamepata muuaji wao, Utata ukazidi
kuibuka, mzee huyu nae anasema kua hakua na nia ya kumuua mke wake Bali
alikua na lengo la kumtisha tu, anadai kua katika maisha yake yote hua
haachi risasi zikae ndani ya bunduki, hivyo anashangaa nani aliyeweka
risasi ndani ya bunduki yake, yeye alifyatua akiwa na uhakika kabisa kua
bunduki yake haikua na risasi ndani hata moja..
Hili Linadhibitishwa na
mke wake ambaye anadai mume wake amekua na 'katabia' ka kumtisha na
bunduki miaka nenda rudi katika ndoa yao wakikorofishana,lakini si siku
hata moja risasi ilitoka hata akifyatua
NANI HASA ALIWEKA RISASI KWENYE HII BUNDUKI? Uchunguzi zaidi unaibua
shahidi anayedai kumuona mtoto wa huyu mzee na mke wako akiweka risasi
kwenye bunduki ya baba yake, Mtoto huyu wa kiume alikua na uhasama
mkubwa na mama yake hali iliyopelekea mama yake kusitisha huduma zote za
kifedha kwa mtoto huyu, mtoto huyu ikafika mahali akatamani kumuua mama
yake,kea kuelewa tabia ya baba yake ya kumtisha mama yake na bunduki
basi akaamua kuiwekea risasi ili baba akimtisha tena mama safari hii
amuue kweli MTOTO HUYU YUKO WAPI? Katika hali ya kusikitisha inafahamika
kua mtoto huyu ndiye hasa marehemu Ronald Opus, Ronald ndie huyu mtoto
wa hawa wanandoa, Risasi alizoweka Ronald Leo hii ndio zimekatisha
maisha yake.
Ronald baada ya kuona maisha yanakua magumu na mtego
alioweka ili mama yake afe hautimii aliamua kujiua kwa kujitupa kutoka
kwenye jengo waliokua wakiishi, lakini risasi iliyofyatuliwa na baba
yake ikamuua!! Hii kesi ilikuja kufungwa kama kesi ya kujiua(suicide)
Kesi hii ilitikisa ulimwengu miaka ya 1994,hali iliyopelekea vyombo vya
habari vilivyokua vikiiripoti kupokea zaidi ya barua 2000 na simu zaidi
ya 400 kutoka kwa watu mbalimbali duniani wakiomba kupewa kibali ya
kuliweka tukio hili katika vitabu vyao au filamu.
**DOWNLOAD MIZIKI MIPYA YA KIZUNGU KWA KUBONYEZA HAPA**
No comments:
Post a Comment