AZIZ ALI PICHANI |
Aziz Ali alifariki mwaka wa 1950 miezi michache baada ya kutoka kuhiji
Makka. Hata kwa mbali katika maisha yake haikumpitikia kuwa mali
aliyoacha nyuma itakuja kutumika katika kupigania uhuru wa Tanganyika
kwanza fedha zake zikitumika wakati wa TAA kisha TANU kupitia mwanae wa
kwanza Dossa Aziz. Itoshe kusema tu gari alilomnunulia mwanae Nairobi
mwaka wa 1947 kama kiliwazo baada ya kukataliwa katika masomo ya urubani
kwa kuwa ni mtu mweusi, ndilo Dossa alilitoa kwa TANU mwaka wa 1954 kwa
ajili ya kumsaidia Mwalimu Nyerere kufanya kazi zake kwa wepesi.
Aziz Ali amekuja Dar es Salaam mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza (1914-1918)
akiwa askari katika jeshi la Wajerumani na baada ya vita aliajiriwa na
Goa mmoja.
Mwajiri wake alipoondoka nchini alimwachia Aziz Ali gari mbili na hizi
ndizo alizokuwa akifanyia biashara hapo mwanzo na kufungua kampuni ya
ujenzi akaajiri mafundi.
Aziz Ali amekuja Dar es Salaam mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza (1914-1918)
akiwa askari katika jeshi la Wajerumani na baada ya vita aliajiriwa na
Goa mmoja.
Mwajiri wake alipoondoka nchini alimwachia Aziz Ali gari mbili na hizi
ndizo alizokuwa akifanyia biashara hapo mwanzo na kufungua kampuni ya
ujenzi akaajiri mafundi.
Kwa hakika jina lake hasa ni Ali Kidonyo.
Hili ndilo jina lake alilojulikana akiwa mtoto na kisha kijana kwao Tanga.
Hili Aziz alipewa na watu wa Dar es Salaam kwa hisani na wema wake.
Yeye alikuwa akitoa fursa kwa watu kumpa pesa kidogo kidogo kama malipo
ya nyumba alizokuwa anawajengea na alikuwa mtu akishindwa kulipa akimpa
muda hadi atakapoweza.
Nyumbani kwake mwezi Mtukufu wa Ramadhani alikuwa akitandika nje majamvi
na kufuturisha hadi watu 100 asiowajua wakija wanafuturu na kuondoka.
Ndipo wakamwita "Aziz" yaani "Mpenzi." Ikawa wakimtaja jina wanatanguliza "Aziz," yaani "Kipenzi chetu Ali."
Kidonyo jina hili la kwao Tanga likafa kabisa.
Aziz Ali alikuwa mcha Mungu sana.
Alikataa kumwanzisha shule mwanae mkubwa Waziri maarufu kwa jina la Dossa hadi kwanza ahitimu Qur'an.
Hii ikapelekea Dossa kuanza shule darasa la kwanza akiwa na miaka 14
akawa darasa moja na Abbas Sykes mdogo wa tatu kwa rafiki yake
Abdulwahid Sykes.
No comments:
Post a Comment