Ninapenda kuwasilisha historia fupi ya 'double agent' Juan Pujol Garcia almaarufu 'Agent Garbo' au Alaric Arabel.
AGENT GARBO NI NANI?
Garbo ni mzaliwa wa Spain(Barcelona) katika familia ya kawaida
kabisa.Akiwa na umri wa miaka saba alipelekwa shule ya bweni ambapo
alisoma kwa miaka minne kabla ya kuhamishiwa shule nyingine ambapo
alikaa kwa miaka mitatu tuu na kuamua kuacha shule baada ya kugombana na
mwalimu.Baada ya hapo alianza kusaidia kazi katika duka la vifaa vya
ujenzi na baadae alisomea ufugaji wanyama na kufanya ufugaji wa kuku
pamoja na biashara nyinginezo kama cinema na hotel ila hakupata
maendeleo/faida.
Mnamo mwaka 1931, Garbo alipitia mafunzo ya kijeshi ya miezi sita ambayo
yalikua ni ya lazima kwa wakazi wote.Garbo hakuyapenda mafunzo ya
kijeshi na alikua akidai kuwa hawezi na hana sifa za kuwa
mwanajeshi.Mwaka 1936, wakati Garbo akifanya kilimo cha ufugaji kuku,
vilianza vita vya wenyewe kwa wenyewe.Jeshi la 'republicans' lilimwomba
Garbo awe upande wao ila alikataa kwasababu baadhi ya ndugu zake
walishakamatwa na hao "republican forces" na kufungwa kwa kosa la
kutokua wazalendo.Garbo alijificha kwa 'girl-friend' wake hadi
alipokamatwa na polisi na kufungwa kwa wiki moja.Baada ya kifungo
alitengeneza kitambulisho cha kugushi kilichomwonesha hana umri unaofaa
kulitumikia jeshi lengo likiwa kukimbia kulitumikia jeshi.
Licha ya kuwa awali alikwishakataa kujiunga na jeshi la republicans,
agent Garbo alifanikiwa kujiunga na jeshi la 'republicans' kwa kutumia
kitambulisho cha kugushi na baadae akafanikiwa kuhamia upande
pinzani.Katika vita hii Garbo anajisifia kwa kutokutumia risasi hata
moja kwa 'republicans' na kwa 'nationalists'.Akiwa katika kambi ya
nationalists Garbo aliadhibiwa(kifungo) baada ya kuonesha huruma kwa
adui yao.Baada ya kutoka kifungoni, Garbo alikutana na msichana ambaye
baadaye walifunga ndoa na kupata mtoto mmoja.Kwa kifupi, Garbo
hakufurahishwa na pande zote mbili za vita ambazo alizitumikia na hii
ilisababisha kuwachukia zaidi 'Nazi Germany' na 'Sovietic union'.
Kutokana na Garbo kutowapenda wanazi, aliamua kuanzisha vita yake
binafsi na Hitler kwa kutumia ushushushu, 'espionnage'.Uamuzi huu wa
Garbo ulikua ni mgumu kwani hakuwahi kupitia mafunzo yoyote ya
ushushushu na hakua na contacts za watu wowote ambao wangeweza
kumsaidia.Akiwa na mke wake, Garbo alienda katika ubalozi wa uingereza
uliokuwepo Madrid akiomba kujitolea kulitumikia jeshi la pamoja 'Allied'
ila maombi yao yalikataliwa mara nne mfululizo.
Baada ya kukataliwa na ubalozi wa Uingereza, Garbo ilibidi ajaribu
kupitia ubalozi wa ujerumani kwa kujifanya kuwa yeye ni m'nazi' na
anaweza kuwasaidia katika kitengo cha ushushushu.Lengo lilikua ni lile
lile la kupambana na Hitler 'from the inside'.Katika ubalozi wa
Ujerumani alikutana na afisa aliyekua akiwasimamia maspy wakinazi
aliyeitwa Federico.Akiwa na Federico, Garbo alimwadisia habari za
kutunga zilizohusisha watu/contacts ambazo Garbo alikua nazo katika
maeneo nyeti ya vita vya pili vya dunia na ili kumshawishi Federico
Garbo alifanya safari ya Lisbon ambapo tayari vita ilikua imechanganya
na watu wanapakimbia.
Akiwa Lisbon, Garbo alijichanganya katika kundi la waportugal waliokua
wanahaha wakitaka kuikimbia nchi yao kutokana na vita.Baada ya kuwepo
Lisbon kwa siku kadhaa, alifanikiwa kukutana na muispaniola mwenzake
ambaye alikua na viza maalumu ya kidiplomasia ambayo ingemruhusu
kusafiri bila shida.Garbo alitengeneza urafiki wa karibu na baadaye
wakiwa katika mgahawa alifanikiwa kumhadaa na kwenda kuingia chumbani
kwake ambapo aliipiga viza ile picha.Baadae aliitumia picha ile
kujitengenezea viza ya kugushi akiwa hapo hapo Lisbon.Federico
alibahatika kuiona ile viza na ndipo alipomuamini Garbo na kumwona
atakua tunu katika kitengo chao na baadaye Garbo alichukuliwa rasmi na
Abwehr, kitengo cha intelijensia cha Ujerumani.Hapa ndipo alipofundishwa
mbinu za kutumia kuwasiliana kwani hakua amesomea ushushushu
kabla.Pamoja na kozi fupi, alipewa wino wa kuandikia, kalamu, pesa za
matumizi n.k
Baada ya kuajiriwa na Abwehr, Garbo alianza kazi rasmi akiwa Lisbon
licha ya kuwa aliwadanganya wajerumani kuwa yupo Uingereza.Aliwapa
taarifa za kipelelezi ambazo alikua akizibuni(taarifa za
kufikirika).Katika taarifa hizi za kufirika Garbo aliwapa wajerumani
taarifa za silaha za waingereza, maeneo ya kambi za kijeshi, safari za
wanajeshi na misafara ya kijeshi kuelekea Malta n.k.Taarifa hizi
alizichakachua kwa kutumia filamu za propaganda, vitabu vya simu,
miongozo ya watalii, ratiba za treni na majarida mbalimbali.Licha ya
kuwa taarifa hizi zilikua ni za uongo, ziliaminika kutokana na namna
zilivyoandikwa kwa mtiririko wa matukio ambayo ilikua ni ngumu kuyatilia
mashaka huku akitumia mtandao wa maagent wengine fake ambao alidai ni
contacts zake katika baadhi ya miji.Katika taarifa zake, Garbo alikua
akitengeneza matukio ya kuonyesha namna baadhi ya maagent fake
walivyosababisha baadhi ya missions zake kufeli na hata pale wajerumani
walipotilia shaka baadhi ya taarifa Garbo aliwasingizia hao maagent fake
kwa ustadi wa hali ya juu na kujiweka katika upande wa kuzidi
kuaminiwa.Katika kutekeleza hili ilifikia wakati akawa anatoa taarifa za
kuuliwa kwa baadhi ya wasaidizi wake(fake) au kuumwa hali
iliyosababisha Garbo kushindwa kutekeleza baadhi ya mission.Wachambuzi
wa uingereza waliokuja kusoma taarifa hizi baadae, hawakuamini kuwa
Garbo hakuwahi kufika uingereza wakati akiandika taarifa hizo.
Baada ya mda waingereza waligundua kuwa kuna mtu anawapa wajerumani
taarifa za uongo.Hii ilikua baada ya Uingereza kuona nguvu kubwa
iliyotumiwa na jeshi la Ujerumani kujaribu kuvizia msafara wa jeshi la
uingereza ambao haukuwepo.Februari 1942, Pujol (au mke wake) alifanikiwa
kuongea na afisa wa jeshi la marekani, Luteni Patrick Demorest ambaye
alitambua kipaji cha Pujol(Garbo).Patrick alizungumza na wenzake
wauingereza na ndipo Garbo alipohamia uingereza na kupokelewa na MI6
kabla ya kuhamishiwa MI5 mwezi Aprili 1942.Hapa ndipo Garbo alipokua
'Double agent' rasmi.
Akiwa Uingereza baada ya kupokelewa na MI6, alipohojiwa kuwa ni kwanini
anapigana against Hitler;kama ilivyokua kawaida yake Garbo alitunga
hadithi iliyomhusisha kaka yake wa kubuni aliyekua anaishi Ufaransa na
ambaye aliuliwa na majeshi ya Hitler kwa kifo cha kinyama.Baada ya
mahojiano ya kuhakikisha kuwa Garbo ni mtu salama, alikabidhiwa kwa
afisa Tomas Harris(mwenye asili ya Spain kama Garbo) aliyekua MI5 ili
amsimamie Garbo na kumpa maelezo ya kazi.
Harris na Garbo wakiwa MI5 waliendeleza kazi aliyokua ameianza Garbo na
waliendeleza ule mtandao wa fake agents.Kilichoongezeka saivi ni kwamba
walituma mtu katika miji yote yenye fake agents kwa ajili ya kukagua
hotel na makasino ambayo yalikua yakitumiwa na hawa fake agents kwa
lengo la kuweza kuelezea maeneo hayo kama yalivyo licha ya kuwa maagent
wanaoishi humo ni wa kufikirika.Garbo na Harris walifanikiwa kutuma
barua 315 kwenda Lisbon kwenye anuani waliyopewa na wajerumani na
kutokana na taarifa za Garbo, ujerumani ilimrank Garbo kama spy wao
namba moja kwa ubora ambaye baadaye walimtunuku 'the iron cross'.Pia
mtandao feki wa Garbo uliwaimpress wajerumani hadi wakaona hamna sababu
ya kuajiri maspy wengine Uingereza, Garbo anawatosha.Garbo alifanikisha
yote haya kwa kuwapa taarifa za uongo kwa asilimia kubwa au taarifa za
ukweli usiokua na athari kwa waingereza.Pia wakati mwingine alituma
taarifa za kweli na zilizokua za hatari kwa waingereza lakini
alihakikisha zinafika kwa kuchelewa ili hatari yake isiwe hatari tena.
Ukiachana na wajerumani, hata waingereza(na jeshi la pamoja kiujumla)
walifurahishwa na kazi za Garbo.Ilipofikia siku ya kumu-attack Hitler
Ufaransa(the D-day) kupitia operesheni iliyobatizwa 'Operation
overload', Garbo alipewa kazi ya kulirubuni jeshi la Hitler juu ya eneo
ambalo uvamizi utaingilia.Uvamizi ulipangwa kufanyiwa Normandy na
Pujol(Garbo) alipewa kazi ya kuliaminisha jeshi la Hitler kuwa uvamizi
hautafanyikia Normandy bali Pas de Calais, Ufaransa.Hii mission ya Garbo
ilipewa jina la 'Operation fortitude'.
'Operation fortitude' ilifanikiwa kwa kutengeneza kambi kubwa ya jeshi
kwa kutumia midoli ambayo iliwakilisha magari ya kivita, shehena za
mafuta, viwanja vya ndege n.k Kambi hii ilikua imewekwa karibu na pwani
ambayo haikua mbali sana na pas de calais, eneo ambalo Pujol alikua ana
kazi ya kuwaaminisha wajerumani kuwa jeshi la mwingereza na mmarekani
litaingilia hapo.Baada ya kutengeneza kambi ya midoli, Pujol aliendelea
kuwaaminisha wajerumani kuwa uvamizi utafanyikia Pas de calais na hata
mashambulizi yalipoanza Normandy aliwadanganya kuwa ilikua ni geresha
tuu na kuwa mashambulizi yenyewe yamepangwa kufanyikia Pas de calais.Hii
ilisababisha Ujerumani kuacha sehemu kubwa ya vikosi vyake Pas de
calais na baadae Hitler kutolewa Ufaransa na kushindwa vita.
Baada ya vita aliachana na mkewe na baadae kwa kushirikiana na MI5
alisafiri hadi Angola ambapo baadae walidanganya kuwa amefariki kwa
ugonjwa wa Malaria na kisha akabadili utambulisho wake na kwenda kuishi
Venezuella ambapo alikua anauza vitabu na zawadi katika duka dogo.Pujol
alifariki mwaka 1988.
No comments:
Post a Comment