Na: bakari bakari jr
Simu: 0659767121
“I don’t see
anyone endowed with talent affirming his desire to go to Spain. It’s a
Championship its great disorder.”
Arsenal Wenger on Henry
Baada ya Thierry Henry kucheza miaka nane ndani ya
kikosi cha Arsenal kambi yao ipo kule Kaskazini mwa London huku akiwa ametwaa
mataji yote ya pale Uingereza nikiwa na maana Premier League, FA Cup na Carling
Cup kwa sasa Carabao, Henry ambaye kafunga mabao 175 kwenye EPL na mchezaji wa
tano wenye mabao mengi. Henry amabye mwaka 1998 alitwaa kombe la dunia akiwa na
kikosi cha Ufaransa na alitwaa euro cup 2000, kitu pekee alichokuwa kabakiza ni
ilikuwa kutwaa taji la UEFA Champion League.
Wakati anahojiwa na waandishi Thierry Henry alikiri
kuwa anataka kutimkia Hispania na lengo kubwa ni kutwaa taji la UEFA Champion
League, Wenger hakuwa na chazaidi kinachoweza kumshawishi Henry kubaki Arsenal ndipo
akasema kuwa “Sijawahi muona mtu yeyote
ambaye amejaliwa na kipaji akijitangaza tamaa yake kwenda Hispania, Klabu
bingwa ni ugonjwa wake” baada ya kusajiliwa 2007 na FC Barcelona mwaka 2009
alitwaa kombe la ndoto yake ya kuchukua taji ya UEFA Champion League ilitimia,
wakati huo Barcelona wanabeba mataji matatu (Treble Won).
Harry Kane ambaye kwa sasa ni mfungaji wa mabao
kwenye kikosi cha Tottenham Hotspur na timu ya taifa akiwa first choice
striker, anafanya kazi ya kupachika mabao ya kila aina kila uchao. Akiwa na
Tottenham Hotspur miaka kumi sasa amefunga zaidi ya mabao 164 kwenye Ligi
mafanikio yake makubwa kwenye timu hiyo ni kuishia nafasi ya pili ya Kombe la
Ligi mwaka 2015.
Harry Kane amekuwa akishinda Player of Month mara
kadhaa na Player of year na hata kutwaa Golden boot katika FIFA World Cup 2018
kule nchini Russia. Lakini mpaka sasa ni miaka kumi yuko Spurs bila taji la
aina yoyote huku Harry Kane anaenda kutimiza umri wa miaka 26 majira ya joto,
ikiwa miaka mingi katumia kuichezea Spurs pasi na taji.
Harry Kane akiendelea kubaki Tottenham hatoshinda
taji lolote kwa sababu ya kwanza Miujiza kwenye soka utokea mara chache na
sababu ya pili Tottenham haina uwezo wa kuleta World class player kwa ajili ya
Ushindani zaidi.
Miujiza ya Leicester City kutwaa EPL katika msimu wa
2015/16 kwa kweli ile ilikuwa miujiza ya kisoka huku timu yao ikiwa well
organized and Committed baaada ya kushika usukani wa Ligi, Lakini pia walikuwa
na bahati wachezaji wao katika msimu 2015/16 hawakupata majeraha jambo ambalo
lilifanya klabu hiyo lichukue kombe la msimu huo. Lakini mchezaji kama Ng’olo
Kante baada ya kuona hali ile haiwezi kujirudia basi akaachana na safari ya Leicester
na kujiunga na Chelsea ambapo pia alitwaa taji la EPL. Swali la kawaida tu
tangu Euro Cup 2004 Ugiriki waishangaze dunia nchi gani tena imefanya hivyo? Miujiza
hii kwenye soka inatokea mara chache tena baada ya miaka mingi, ndio maana
wakina Kante, Riyadh Mahrez baada ya kufanya miujiza hiyo mmoja akaenda Chelsea
mwingine akatimkia Man City.
Kwa hali ya Tottenham haina uwezo wa kumleta
mchezaji mwenye thamani ya zaidi euro million 60 kutokana na soko la usajili
ulaya lilivyokuwa, kama timu inashindwa kuleta hawa World class Player majukumu
ya timu anakuwa nayo Harry Kane ambapo akipatwa na jeraha basi fomu nzima ya timu
inapotea na kuanza kupoteza michezo yao na ndio maana wachezaji kama Luka
Modric aliondoka mapema baada ya kupata ulaji Real Madrid, lakini pia Gareth Bale
alitambua hilo akaona ni vyema kurukia Meli ya Madrid for Career growth and
development, Kyle Walker nae katimkia Manchester City tangu 2017, hawa wote
wana mataji Modric na Bale wametwaa UEFA Champion League, La Liga, Club World
Cup, Copa Del Rey. Kyler Walker ana taji la Premier League na Vikombe viwili
vya Ligi.
Harry Kane uenda anatamani sana kuondoka timu yake
hiyo ya utotoni Tottenham lakini anawafikiria maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo
ambayo ambao wote wanamuangalia yeye kwa furaha huku wakimuimbia nyimbo ya “he’s one
of our own”, hali hii inakuwa kama legend wa Udinese Antonio Di Natale ambaye
alikubali kubaki Udinese pasi na kushinda taji lolote. Di Natale akiwa na 25
kabla hajafika miaka 30 alishafunga mabao 47 kwenye Serie A katika
misumu mitano kuanzia 2009 mpaka 2014 Di Natale alishafunga mabao 120 kwenye
ligi akiwa na miaka kati ya umri wa miaka 31-36 akiwa mchezaji wa sita kwa
mabao kwenye seria A. Lakini alikataa kuondoka mara zote huku akisisitiza kuwa
anabaki Udinese. Au anataka kuwa kama Steve Gerald ambaye juu ya kutakiwa na
klabu nyingi kubwa Ulaya alibaki Liverpool kuichezea kwa mapenzi yake yote huku
akitwaa taji la Klabu bingwa Ulaya jambo ambalo Tottenham hawawezi kufanya
japokuwa wako kwenye hatua ya robo fainali.
Kama Kane anataka kuendelea kusikiliza nyimbo “he’s
one of our own” wakati akiwa katika uwanja wa White Hart Lane basi aendelee
kubaki Spurs lakini kama anahitaji mataji basi akusanye virago vyake akaanze
maisha mapya nje ya Spurs, kama walivyofanya wakina Henry, Van Persie, Mahrez,
Bale, Modric, Walker wakati sasa wa kubadilisha mabao yake yazae mataji.
No comments:
Post a Comment