ANALYSIS: UCHAMBUZI WA KISAYANSI HUYU NDIYE BINGWA WA UEFA CHAMPION LEAGUE - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Saturday, May 26, 2018

ANALYSIS: UCHAMBUZI WA KISAYANSI HUYU NDIYE BINGWA WA UEFA CHAMPION LEAGUE

 

Na:Bakari Jr
Simu:0659767121

Unafikiri uchangamfu unaweza ukauzidi uzoefu katka maisha? Usiku wa leo katika mji wa Kiev capital town katika nchi ya Ukraeini kutakuwa na fainali ya ligi ya mabingwa kati ya Real Madrid vs Liverpool FC (2018 Champions League final).

Kikosi cha Real Madrid kimekuwa na uzoefu mkubwa wa kucheza michuano na fainali (na kutwaa taji) katika michuano hii mikubwa ya vilabu vya Ulaya na kuwa na rekodi ya kuchukua taji hilo kwa takribani mara kumi na mbili, huku wenzao Liverpool wakitwaa mara tano, Yote tisa kumi ni pale katika miaka minne iliyopita Real Madrid imetwaa taji hilo mara tatu.

Kuwepo kwa wachezaji wenye uwezo mkubwa kwenye kilabu cha Real Madrid pia wenye uzoefu wa kutosha katika michuano hii kunaipa faida kubwa sana klabu hiyo, Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Sergio Ramos au Kaylor Navas ni wachezaji amabo naweza sema wanauwezo mkubwa sana wa kinyota (Horoscope) mpaka kufanya timu hiyo itwae taji mara tatu katika fainali nne zilizopita.

 

Lakini ulishawahi kujiuliza kuhusu nyota ya kocha wa Real mkongwe Zinedine Zidane ambaye amefanya makubwa sana katika Kombe hili?.  Ukiunganisha nyota ya Zidane pamoja na wachezaji wake inaonyesha wazi kuwa wana football fraternity(udugu wa kisoka) ambao unatoka katika sayari ya Zohari, Zohari ni sayari ya  uvumbuzi na usumbufuthe na imeadhimishwa. Hii ni sababu kwa nini Real imekaa juu kwenye Ligi hiyo ya mabingwa kwa miaka mingi.

Ukweli ni kwamba Madrid katika kikosi chao wana watu ambao ni wana nyota ya mataji, Ili ujiridhishe ili angalia fainali zote wanakuwa undermined lakini wanatwaa kombe hilo. Lakini ni ngumu sana kwa kocha wa klabu hiyo mfaransa Zidane kutwaa taji hilo kwa mara  tatu mfululizo.

Kikubwa ni pale Madrid wanapoenda kukutana na timu ya vijana chipukizi, kama ni mbegu ndio kwanza inachipua, Hakika inafurahisha, Unajua nini wengi wa vijana hawa ambao wanachezea Liverpool ni kuwa wamezaliwa mwanzoni wa miaka ya 1990, hakika vijana hawa pamoja na Kiongozi wao bwana Jurgen Klopp wapo katika Sayari ya Pluto. Kwanini Pluto, kwa kuwa wachezaji hawa wanahitajika wazaliwe upya, Wafanye mageuzi na mwishowe wafanye mabadiliko.

Image result for LIVERPOOL SQUAD 2018

Watu wengi wanadhania kuwa uchangamfu wa wachezaji wa Liverpool unaweza kupeleka Chalenji za kutosha katika kikosi cha wazoefu ambacho tayari kimejijenga, huku wao Liverpool wapo katika kuzaliwa upya, wafanye mageuzi na mabadiliko. Liverpool ni Pluto na  Real Madrid ni Uranus, Siku zote Pluto ni wachangamfu na wana nguvu kutokana na umri wao mdogo na ndio maana tunategemea kuwa Real Madrid wanaweza kuishangaza dunia. Ikumbukwe kuwa Klabu ya Liverpool imepitia mabaya mengi huku ikikosa kucheza michuano hiyo kwa miaka kadhaa timu kufanya vibaya kwenye ligi na kukosa taji la Ligi, Hakika bado vijana hawa wa Pluto hawana uwezo wa kusgangaza dunia ila wanahitajika wazidi kuzaliwa upya na kufanya mabadiliko alafu waje tena baadae.


Achana na viwango vya karibuni walivyokuwa navyo wachezaji wa Liverpool, unadhani Mohammed Salah, Jordan Henderson, pamoja na Sadio Mane wanaweza kuibuka washindi mbele ya wachezaji wa Real Madrid ambao wapo kwa miaka mingi? Wanachezaji wenye uzoefu, wana uwezo wa michuano hiyo. Unadhani beki ya Real itashindwa kwenda kumdhibiti Salah? Miaka baadae Salah atakuwa bora Zaidi katika mpira sio kwa leo. Hakika wazi kuwa Jurgen Klopp na Liverpool watatoka vichwa chini.
 




No comments:

Post a Comment

Pages