REVIEW: Ujio wa Legends of Tomorrow Season 4 - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Friday, July 6, 2018

REVIEW: Ujio wa Legends of Tomorrow Season 4


Welcome back... Katika sehemu hii ambapo tunafanya marejeo ya filamu (Movie review) kuangalia ni kitu gani tumeweza kujifunza, kulikuwa na makosa gani, waliwezaje kutengeneza na vitu mbali mbali kuhusu movie husika.

Leo hii nimekuletea taarifa kuhusu series ya Legends of Tomorrow ambayo imesheheni superheroes kibao kutoka DW huku Wentworth Miller akiwepo (Michael Scofield), Victor Garber, na Franz Dramer Lakini baadae Cw wakaingia kati  kuleta watu kama Grant Gustin (The Flash) na mtaalamu Oliver Queen mzee wa mishale, na kufanya Series hiyo kuwa kali zaidi.

Mpaka sasa hivi Imetoka jumla ya Misimu mitatu(Season tatu), Lakini kwa sasa taarifa inasema kuwa kampuni ya DW italeta mzigo huyo baadae mwaka huu.

LINI ITATOKA SEASON FOUR

Kumbuka kuwa season 3 iliishia pale ambapo Gary na John Constantine (Matt Ryan) wakitafuta team ya watu ambao watapambana na magical threat.

Ujio wa Season four ya Series hii imetangazwa kuwa ni tarehe 22 mwezi oktoba mwaka 2018, Episode one yake imepewa jina la "The Virgin Gary", itarushwa kupitia CW.

Keiynan Lonsdale hatokuwepo tena

Mtaalamu Keiynan Lonsdale, ambaye amecheza kama Wally West / Kid Flash ambaye ameonekana ana kasi kuliko ya Barry hatowez kuwepo tena katika msimu huu wa nne, Lakini Barry atakuwa ndio mwenye kasi zaidi ya Wally baada ya Barry kumzuia Wally, Lakini tumeambiwa kuwa anaweza kurejea tena katika Msimu wa tano (Season 5), Pia kuwepo kwa Matt Ryan katika msimu huu wa nne.

No comments:

Post a Comment

Pages