Katika soka kuna wachezaji wengi wenye vipaji wamezaliwa lakini kwa bara la afrika kuna wachache ambao wanajulikana kutokana na kucheza timu au ligi kubwa dunia kama vile LA LIGA, SERIE A, au EPL. Lakini bwana Sibusiso Wiseman Zuma amezaliwa 23 Juni 1975 huku nchini afrika kusini alicheza soka akiwa na klabu ya nyumbani kwao Afrika Kusini akicheza kama kiungo mshambuliaji, mshambuliaji au winga ya kulia. Wasifu wake kwa ufupi ni:
"Zuma ilianza wasifi wake katika klabu za Afrika Kusini kama vile Mighty Pa, African Wanderers na Orlando Pirates. Mwezi Juni mwaka wa 2000, alijiunga na klabu ya Kideni ya FC København, ambapo alijiendeleza kama mchezaji. Aliisaidia klabu yake kushinda taji la ligi ya Kideni kwa mara yake ya pili na aliteuliwa kuingia katika “hall of fame” ya klabu kutokana na jitihada zake bora katika msimu wa 2004-05, na mwaka wa 2001 Zuma aliteuliwa katika nafasi ya 29 katika tuzo la mwanakandanda bora wa FIFA wa mwaka wa 2001. Baada ya miaka 5 ½ katika klabu ya FC København, Sibusiso Zuma aliuzwa kwa klabu ya Bundesliga, ambayo ni ya ligi ya Kijerumani, Arminia Bielefeld kwa kitita cha yuro milioni moja mnamo Julai 2005". "CHANZO WIKIPEDIA"
Moja ya magoli yake lakukumbukwa zaidi ni lile dhidi ya Brondby

No comments:
Post a Comment