Real Madrid hakuna Galactico, Hakuna Superstaa wala Hakuna Mashabiki - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Tuesday, August 21, 2018

Real Madrid hakuna Galactico, Hakuna Superstaa wala Hakuna Mashabiki

a group of people standing next to a man: Real Madrid Ronaldo fans 19082018

Na: Bakari Ally
Simu: 0659767121

"Hakuna mchezaji asiyenunulika"
Mwanzoni mwa mwaka 2000 dunia ilishuhudia mabadiliko ya uongozi wa klabu ya Real Madrid,  Lorenzo Sanz, akipoteza kiti chake cha urais mbele ya Fiorentina  Pérez, huku Perez akiwa amehaidi kuirudisha Sera ya Galactico klabuni hapo, Huku akihaidi kila dirisha la usajili la kiangazi kuleta mchezaji ghali mwenye uwezo mkubwa kiuchezaji.

Nimeanza na kauli ya Rais wa Klabu ya Real Madrid Fiorentina Perez akiwa anasema hivyo mwanzoni wa miaka ya 2000, hii ilikuwa akisisitiza kuwa hakuna mchezaji ambao wao watashindwa kumsajili kutokana na kuwa na pesa nyingi za uhamisho, hii alikuwa anasimamia sera ya Galacticos "Galacticos Policy" kuwa timu hiyo iko tayari kumsajili mchezaji yeyote kutoka sehemu yoyote ile duniani kwa pesa yoyote ile, Kwenye sera hiyo ndipo akaonyesha jeuri Fiorentina Perez akamsajili Luis Figo kwa kiasi cha €60 million kutoka kwa wapinzani wao Barcelona, Mwaka 2001 wakamsajili Zinadine Zidane kwa €77.5 million, huku 2002 walimsajili De Lima kwa €46 million kutoka Inter Millan, Baadae 2003 walimsajili David Beckham kwa €37 million akitokea Manchester United.

Image result for zidane, raul, beckham

Kutokana na usajili wa mastaa kibao basi wazi kila mtu alikuwa anatamani kuiona klabu hiyo ikiwa inacheza na mvuto wa mastaa mbali mbali wakiwa ndani na nje ya uwanja, Orodha ndefu sana lakini mwisho wa siku Ndipo alinunuliwa Mchezaji wa mwenye asili ya kireno anayejulikana kama Cristiano Ronaldo, Ronaldo sio tu ni Galactico lakini pia ni Supastaa wa klabu kuanzia ndani na nje ya Uwanja, kila mtu alikuwa anaiangalia Real Madrid kwa ajili ya kumuona Ronaldo akiwa anacheza.

Hakuna Supastaa


Ronaldo ameondoka Real Madrid kipindi cha usajili kilichopita tumeshuhudia staa huyo akiondoka klabuni hapo, ambapo alidumu kwa takribani miaka tisa. Lakini Klabu ya Real Madrid haijanunua mchezaji yoyote ambaye anaweza kuziba pengo lake, Madrid walikuwa wanahitaji saini ya Neymar, Mbappe na Hazard kutoka Chelsea lakini mpaka dirisha linafungwa hakuna ambaye amesajiliwa mpaka dirisha limefungwa.

Image result for madrid cf

Klabu ya Real Madrid imeanza maisha ya bila kuwepo na staa wao Cristiano Ronaldo, ambaye ameiongoza timu hiyo kwa miaka tisa na kuifungia klabu hiyo mabao 450 katika michezo 438 akiwa na Real Madrid, Lakini tangu kuondoka kwa supastaa huyo wa kireno timu ya Real Madrid haijafanya usajili wowote kwa ajili ya kuboost safu yao ya ushambuliaji hu8ku wa sasa wakiwa wanawategemea Karim Benzema, Marco Asensi pamoja na Gareth Bale kuiongoza safu ya ushambuliaji wa klabu hiyo.

Kocha mpya wa Timu ya Real Madrid Julen Lopetegui amesema kuwa Mshambuliaji Gareth Bale ndio atapewa kuiongoza klabu hiyo, Jana katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ncini hispania maarufu kama LA LIGA BBVA, tumeona Gareth Bale akifunga goli la pili katika mchezo huo na kuifanya Real Madrid kuchomoka na ushindi wa goli 2-0.

Tatizo sio kupata ushindi lakini Ronaldo ni zaidi ya mshambuliaji, Ronaldo ana mashabiki wengi ambao wanapenda kumuona akiwa nje ya maisha ya soka hadi katika uwanja, Wakati Ronaldo amejiunga na Juventus wakati wa Usajili kuna idadi kuwa ya Followers wa Real Madrid kwenye ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo waliacha kui-follow akaunti.

Washabiki watalii na wakereketwa


Kwenye mchezo wa soka kuna mashabiki wa aina mbili kuna Mashabiki Wakereketwa na Washabiki Watalii(kutokana na Criteria zangu), Mashabiki wakereketwa ndio hawa ambao wao wamejitolea kushangilia timu hiyo lakini hawa mashabiki watalii hawa wao wanaenda kuangalia mechi ambayo hakuna timu yao lakini wanaenda kuiangalia mechi kutokana na uzito wa mechi hiyo au kuna mchezaji/wachezaji wanawafuata kuwaona.

Image result for madrid cf fans

Lakini sio kuangalia upande wa Ronaldo, Kocha aliyepita mfaransa Zinadine Zidane alikuwa ni moja ya supastaa kila shabiki alihitaji kumuona, watu wengi walikuwa wanaenda Uwanjani kutokana na Influence yake kutokana alikuwa na uwezo mkubwa wa kuiongoza timu hiyo na kupata matokeo pamoja na mataji, Hali hii ilimfanya kila mtu aweze kufika uwanjani kuiangalia klabu ya Real Madrid.

Mashabiki ambao wao sio wapenzi wa Real Madrid lakin walikuwa wanafuatilia matukio yote ya klabu hiyo, kujua taarifa, matokeo, mechi nk hawa ni mashabiki watalii walikuwa kwa ajili ya Cristiano Ronaldo, Lakini kwa sasa hao pia hawaonekani uwanjani kutokana na kutowepo kwa Ronaldo kikosini, Hakuna mchezaji wa Real Madrid ambaye anaweza kuvutiwa kuangaliwa kama Ronaldo.

Viti wazi katika Uwanja wa Bernabeu & Hakuna Galactico


Jana msimu mpya wa LA LIGA umeanza huku klabu ya Real Madrid hakika jana imeonekana imepoteza mashabiki kuanzia mashabiki wao(wakereketwa) mpaka washabiki wataliii, Mahudhurio yao uwanjani yamekuwa machache sana ukilinganisha na miaka 10 iliyopita jumla ya watu 48,466 ndio wameweza kuhudhuria mchezo wa jana idadi hii ni ndogo ukilinganisha na ile ya siku ya Simba day kati ya Simba SC vs Asanteh Kotoko ambao mahudhurio ni 52,000.

Real Madrid's Welsh forward Gareth Bale kicks the ball past Getafe's Uruguayan defender Leandro Cabrera (L) during the Spanish League football match between Real Madrid and Getafe at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid on August 19, 2018. (Photo by JAVIER SORIANO / AFP)        (Photo credit should read JAVIER SORIANO/AFP/Getty Images)

Kwa sasa Real Madrid haina Supastaa ambaye watu wanaweza kupeleka jicho lao kuiangalia klabu hiyo maana kikosi cha kwanz (first eleven) ndio kile ambapo Zidane alikuwa anatumia huku wachezaji wote ambao waliingia kutokea benchi ndio wale walikuwa kwenye wanatumika na Zidane.

Sura mpya kwenye kikosi hiko ikiwa Golikipa Thibaut Courtois kutokea klabu ya Chelsea pamoja na mchezaji kijana wa kibrazil Vinicius Junior wakiwa walikuwa benchi.

Kwa kweli kocha wa Real Madrid ameamua kuleta staili ya Tiki Taka, ambapo mashabiki wengi tumeshuhudia pasi nyingi zikipigwa zaidi ya mia saba huku 91% ya pasi zikiwa zimemfikia mlengwa, huku wakiwa na umiliki wa mpira (Ball possession) 78%.

 Image result for madrid cf troph

Lakini kitu pekee amacho klabu ya Real Madrid na kocha wake wanaweza kufanya ili waweze kuirudisha klabu hiyo kama zamani ni kushinda mataji na  wala sio kuhesabu idadi za pasi au staili ya klabu hiyo inavyocheza uwanjani, kwa sasa Real Madrid haina Galactico ambaye amesajiliwa wala Supastaa wa ndani na nje ya uwanja na pia imepoteza mashabiki.

No comments:

Post a Comment

Pages