NINAVYOAMINI MIMI | ATLETICO MADRID HAWABIPU WANAPIGA,UKITAKA WANAKUUZIA - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Wednesday, April 30, 2014

NINAVYOAMINI MIMI | ATLETICO MADRID HAWABIPU WANAPIGA,UKITAKA WANAKUUZIA

Na: Bakari Ally
Simu:0682004504

Related image

Maisha yapo ya kasi sana kuna kipindi watu wakisema kuna tofauti tofauti moja tu kati ya V.P.L na La Liga tofauti yenyewe La liga wengi watu weupu wakati Tz v.p.l wenyewe waafrika lakini tanzania kumeibuka timu inaitwa azam na sasa kuna mbeya city wamekuja kuwapa chalenji simba na yanga huku pia La liga spaini kuna timu imefufuka inaitwa atletico madrid nao wamekuja kuwapa chalenji real na barcelona

Mwanzoni mwa ligi tuliowaona atletico wapo vizuri huku watu wengi wakisema hizo ni nguvu za soda kama za southamptom,napoli na As roma lakini bado wapo Atletico madrid wapo kileleni mwa ligi nani anaweza kuamini, Na raisi wa timu amesema kuwa mwaka huu mpaka kieleweke kitu jirani zao real madrid wapo vizuri lakini kuna muda wanafungwa na timu usizozijarajia,barcelona wanasuasua kidogo kitendo cha atletico kuongoza ligi hatua hizi za mwishoni ni wazi kuwa walikuwa HAWABIPU BALI WANAPIGA tena simu yao ipo fulu dola haiwezi kukatia wakikupigia,nani alitarajia kama Atletico wataingia robo fainali ya UEFA wametoka katika kundi lenye timu ngumu pia 16 bora wamekutana na Ac Milan lakini milan alichezea kichapo mpaka sasa wemetinga robo na wamekutana na barcelona nao wawe macho wanaweza wakaumbuliwa kwa kuwa HAWABIPU WAO WANAKUPIGIA Moja kwa moja.

Hivi unamjua yule mtaalamu wa kupachika mabao raia wa spaini anachezea Chelsea huyo sio mwingine ni Fernando torres au wahispain wanamuita El Nino, Walimuuza wao kwenda liverpool akiwa kwenye kiwango imara HAWANA HIYANA UKITAKA WANAKUUZIA.

Je unamjua yule mruguary aliekuwa anacheza nyuma ya luis suarez kwenye world cup 2010 pale afrika kusini ni diego forlan baada ya torres kuuzwa ndipo wakamnunua kutoka virrareal alikuwa pia na yule striker wa kiargentina Kun Aguero walitengeneza pertnership ya kutisha kulikuwa na muargentina mwingine akiitwa MAXI RODRIGUEZ huku golini kulikuwa na mtoto wa kìhispain ambae anaweza kutumia urefu wake akiwa golini kwa kupangulia mipira ya chini ni David de gea,maxi aliuzwa liverpool huku de gea,aguero na forlan wakiuzwa mwanzoni mwa msimu wa 2011/12 baada ya mechi ya super cup dhidi ya Inter milan,huku de gea akitua man united na aguero kwenda man city mwenzao Forlan alienda inter milan watu wengi wakasema timu imekufa lakini mwaka 2010 walimleta mtoto wa kibrazil anaechezea timu ya taifa ya spaini ni DIEGO COSTA kutoka braga ya nchini ureno lakini wakamwambia muda wako wa kucheza bado wakampeleka kwa mkopo,baadae wakamleta fundi kuto PORTO ambae ni Mkolombia ni RADAMEL FALCAO kila mtu anamjua falcao aliwai kuwa chalenji MESSI na CR7 Kwenye kupachika magoli huo ni msimu wa 2012/13 ulipomalizika msimu As monaco wakamtaka kwa roho safi atletico wakamuuza wao wakamsajili DAVID VILLA kutoka BARCELONA lakini mara nyingi anatumia kuuguza majeruhi lakini Diego costa amekuja kuwa mpachikaji hatari baada ya kuondoka Falcao na kwa sasa Costa yupo sokoni timu yoyote itakayofika dau atauzwa.WAO HAWANA HIYANA UKIMTAKA MCHEZAJI WANAKUUZIA

Wao kazi yao wanaangalia je nani anauzwa?Na nani anakuja kuziba pengo lake kwa pengo la diego costa kinda Oliver torres ndio ataziba pengo lake.UKIMTAKA MCHEZAJI WANAKUUZIA HAWANA HIYANA

FORGIVE ME

No comments:

Post a Comment

Pages