VAR NI NINI? NA INAFANYAJE KAZI? MAENEO GANI YANAHUSISHA VAR? - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Monday, February 19, 2018

VAR NI NINI? NA INAFANYAJE KAZI? MAENEO GANI YANAHUSISHA VAR?

Makala na: Bakari JR
Simu: 0659767121

Tokeo la picha la VAR help referee
REfa akiangalia tukio kupitia VAR teknoloji
VAR( Video Referee Assistance) Hii ni teknolojia ambayo imeletwa na chama cha marefa kupitia International Football Association Board (IFAB), ikiwa na lengo la kusahisha refa wa kati katika maamuzi yake kupitia video. Kwa sasa mechi nyingi zinakuwa na waamuzi wanne namaanisha refa wa kati, ma-lines men wawili pamoja na fourth official, japokuwa kuna baadhi ya michuano kunakuwa na marefa nyuma ya magoli.
Endelea kusoma
Kutokana na makosa ya kibinadamu chama cha maamuzi wasaidizi waliomba hii kuwepo kwa refa wa tano ambaye yeye atakaa katika, Video akiwa na haedsett kwa ajiri ya kuwasiliana na refa wa kati.

Vitu gani vinaangaliwa na Video Referee Assistance?

Kwa sasa teknolojia hii ya VAR inaonyesha mapitio ya Vitu vinne, moja ni Goli, Penati, Kadi nyekundu na nne ni Kutambua makosa (mistake identity).


Namna gani VAR inafanya kazi?

Kwa kutofautisha kuna vifupisho nitatumia ili ulichanganye, VAR ni Video referee assistance maaana yake ni ile kamera inayorekodi tukio, wakati AVAR kirefu chake ni Assistant Video Assistance Referee ikiwa na maana kuwa ni yule mtu ambaye anaopareti na VAR na kumuambia refa wa kati, VOR ni Video Operation Room ni chumba maalumu ambacho AVAR anakaa ambapo anakuwa na mtu anaitwa RO huyu ni Replay Operator, hawa wakina AVAR ni refa tu kama wengine so hawezi au ana ufinyu kujua kuhusu na mitambo ya kurusha mpira kwahiyo RO ni anamsaidia kufanya marejeo ya tukio analohitaji kuliona, pia OFR maana yake ni On-field referee mwamuzi wa kati ambaye anachezesha mechi.

Mchezaji wa Arsenal OXlade Chamberlain aligusa mpira kwa mkono
katika mchezo dhidi ya chelsea 


Angalia hiyo picha hapo juu ni mwaka 2014 ambapo Oxlade Chamberlain alishika mpira kwa mkono lakini kwa bahati mbaya refa alimpatia kadi nyekundu Kieran Gibbs, maana ake hiyo ni error ya OFR lakini kule AVAR atafanya review ambapo akijua kama maamuzi sio sahihi kadi inafuta anapatiwa anaestaili.
Referee Andre Marriner sent off the wrong player in a remarkable case of mistaken identity, sending Keiran Gibbs off instead of Alex Oxlade-Chamberlain who used his hand to push a shot away from goal on March 22, 2014
Bahati mbaya refa alimpatia kadi nyekundu Kierani Gibbs 

Namna gani wanawasiliana?

Hapo tumeongelea hilo tukio sasa ni vipi wanawasiliana ni kwamba kama refa wa kati (OFR) atakuwa hana uhakika atamuuliza AVAR kuhusu hilo tukio, na AVAR akiwa kimya maana ake OFR yuko sahihi na maamuzi aliyotoa hii ni "silent check" na kama akigundua kuna makosa atamuambia ili kumsahisha.


AVAR akimuambia OFR nini kinatokea?



Tokeo la picha la var
Hapa kuna AVAR nina maanisha ni refa by professional na RO ambaye sio refa ila ni technician 
Kama tukio limetokea na VAR imemuambia refa wa kati kuwa kuna tatizo hili refa wa kati anakuwa na machaguo matatu kwanza ni anaweza kubadili maamuzi yake na kufuata VAR, pili kama akiona inamtatiza uwanjani kuna sehemu panaitwa Referee Review Area (RRA) hapo ataenda kuangalia marudio ya tukio akiwa na Review assistant (RA) au chaguo lake la tatu ni kusema nina amini maamuzi yangu so haendi kuangalia video.

Vitu gani VAR inasaidia goli likifungwa?

Tokeo la picha la why var refuse mata goal
Man utd vs Huddlsfield
Nimesema kuwa VAR inaangalia vitu vinne kwanza goli, pili penati, tatu kadi nyekundu na makosa (mistake identity).
Kwa upambe wa goli VAR inaangalia vitu kama kabla ya goli kufungwa kulikuwa na offside kama iliwepo goli linakataliwa, kabla ya goli kufungwa mpira ulitoka? ikiwa ndio goli linakatiliwa, je kuna faulo ilifanyika kabla ya kufunga? na wakati huu haya maamuzi yanaweza kuchukua kama sekunde 30-40.
Matumizi ya VAR katika kadi nyekundu hapa inafanya kati kwa zile direct red card maana ake kama ni kadi ya njano VAR haihusiki ata ikiwa ni kadi ya pili ya njano, na kuna instance ambapo VAR ina mshauri refa hapa kwanza uigaji, kufunga goli kwa mkono, na ikigundulika umemrudishia mwenzako(kisasi).
Tokeo la picha la var
Hii ni penati baada ya kuangalia kwenye video assistance referee hii ndio ishara inayotumika kuchora mstatili hewani
Kwa upande wa penati inaonyesha kama mchezaji kafanyiwa faulo nje au ndani ya eneo la kumi na nane. Kama refa ataenda kuangalia review ya video akaona kuna penati basi atanyoosha vidole viwili, baada ya kidole kikubwa kinachofuatia na ataonyesha alama ya mstatili (rectangle) afu atatoa penati, hii ina maana kuwa ameona kwenye VAR.

Nini kitatokea endapo wachezaji au kocha atamzonga refa?



Kama mchezaji atasema aende kwenye video ambayo refa anaenda kuangalia, refa ana haki ya kumpa kadi ya njano na hii ata kama ni mchezaji wa akiba atapata kadi ya njano, na kama kocha atasema akamsonge refa kwenye VAR ya uwanjani basi ataonywa na kama atatoka kwenye kiboksi chake kwa mita tatu atatolewa uwanjani so ataenda back stage.

Historia fupi 

Kwa mara ya kwanza kutumia kwa VAR katika mechi ya uingereza ni Brighton v Crystal Palace FA Cup ndio walianza kutumia hii teknolojia.
Lakini kwa dunia nzima ilitumika katika mchezo wa Major League Soccer lakini pia ilitumika mwaka 2016 katika fainali za Club world cup,lakini nchini Australia ndio ligi ya kwanza kutumia mfumo huu katika professional league. 





























**DOWNLOAD MIZIKI MIPYA YA KIZUNGU KWA KUBONYEZA HAPA**

No comments:

Post a Comment

Pages