KUMBUKUMBU | HAMZA BENDELLADJ "THE SMILLING HACKER" - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Thursday, April 12, 2018

KUMBUKUMBU | HAMZA BENDELLADJ "THE SMILLING HACKER"

Na-Bakari jr
Simu-0659767121

Tokeo la picha la HAMZA BENDELLADJ

"Siku ya tarehe isiyojulikana, lakini inaweza kuwa tarehe 21-02-2011 mpaka tarehe 24-02-2011 , tarehe kamili haifamiki na mahakama ya Grand Jurry katika wilaya ya Georgia and sehemu nyingine, Mtuhumiwa HAMZA BENDELLADJ aka Bx1 alisaidiana na kusababisha na wenzake wanaojulikana na wasiojulikana na Mahakama, kwa akili zake timamu na kwa hiari yake alidukua kompyuta bila kuruhusiwa na akapata taarifa kutoka kwenye kumpyuta inayolindwa kwa lengo la kujinufaisha kiuchumi"-Maneno hayo yakisema na hakimu mahakama ya Georgia chini ya Sally Quillian Yates

Mwishoni hukumu inatoka baada ya HAMZA BENDELLADJ kywa na makosa 14 yaliyomtia hatiani huku akihukumiwa miaka 15 jela pamoja na mshirika wake aliyejulikana kwa jina la Aleksander Andreevich Panin aka Gribodemon kuhukumiwa miaka tisa jela. 

JE HAMZA BENDELLADJ NI NANI?

 Tokeo la picha la HAMZA BENDELLADJ
Siku ya Ijumaa ya tarehe 3 June 1988 katika eneo la Tizi Ouzou, Kouba, nchini Algeria ndio DANIEL HAMZA BENDELLADJ elimu yake alisomea katika nchi yake ya Algeria na alikuwa na Stashahda ya Uhandisi wa Kompyuta, Lakini katika kuhitimu Stashahada yake aliwahi kufanya kazi ya Kompyuta maintainance kwa muda wa miaka mitatu. Jina lake la Code ni Bx1, pia waandishi wa habari walimpa jina la Smilling hacker kwa kuwa muda wote anatabasamu japokuwa alikuwa chini ya polisi.
Hamza alikuwa na mke pamoja na mtoto mmoja lakini haijulikani wanaishi wapi.
Baada ya kutoka kufanya kazi kama computer maintainance baadae Hamza alianza kazi ya kudukua (hack) kompyuta za mabenki mbalimbali na kuiba pesa za kusafirisha kwenye akaunti yake, Aliwezeje kufanya hivyo?
Hamza alitengeneza Trojan Horse Virus, ambapo alikuwa anaingia kwenye kompuyta yoyote ile na kuiba taarifa za watumiaji (username & password)  baadae alikuwa na system ya  ATS(Automated Transfer System-along Zues trojan) ambayo kazi yake ni kuhamisha pesa automatically mara moja tu atakapo ingia(account login).

Inahamika kuwa alifanikiwa kudukua benk na taasisi nyingine za kifedha jumla 217 na aliiba zaidi ya dola million mia tatu, lakini katika akaunti yake alikutwa na dola million kumi. Pia Hamza alikuwa ni moja ya unethical hacker(wadukuzi wasio na maadili) ambayo orodha ilitolewa na MICROSOFT kuwapa polisi wa Marekani.

MAISHA YA HAMZA
Hamza alikuwa anaishi katika Grand hotels lakini pia alikuwa anaishi maisha ya kifahari ambapo alikuwa anasafiri na ndege siti za first class. Baada ya kuanza kutafutwa na maaskari wa kimarekani Hamza alikuwa kila siku anafanya kazi ya kubadili IMEI namba ya simu yake aina ya Iphone na kubakia anonymous.

Hamza alikutana na rafiki yake mwenye asili ya kirusi Aleksander Andreevich Panin kwa kushirikiana wakatengeneza software iliyojulikana kama SPYEYE ambayo ilikuwa inaiba pesa, Pia alikuwa anawauzia wadukuzi(hackers) wengine na ilikuwa inatiumika kama BOTNET.

Nini BOTNET? Kwa lugha ya kompyuta bot maana kifupi cha ROBOT na net ni NETWORK kwahiyo botnet ni mtandao wa maroboti ambao unaunga idadi ya watu mfano kumi alafu wanakuwa controlled na server/computer moja.
kirusi hiki cha SPYEYE inahaminika kilidukua na kuathiri zaidi ya kompyuta million hamsini. Lakini mpaka leo hii software ipo katika black market inauzwa kwa dola elfu kumi.

Kwa pamoja Hamza na rafiki ake Panin walikuwa na kundi la chini(underground group) ambalo ni kikundi cha hackers ambao ni unethical inaitwa Darkode.com, pia wawili hawa walijulikana kama legend katika dark world  (rejea hapa kuhusu dark world).

PESA ZA HAMZA ZIKO WAPI?
Hamza aliiba taasisi karibu 217 lakini alikuwa na utajiri wa dola million kumi, pesa nyingi alikuwa anaopeleka Algeria, sehemu yenye vita Syria, Palestina nk kwahiyo yeye chache tu ndio alikuwa anatumia kati ya nyingi alizoiba..

KUKAMATWA KWA HAMZA

Tokeo la picha la HAMZA BENDELLADJ
Hamza alikamatwa nchini Thailand katika uwanja wa ndege wa SUVARNABHUMI ambapo alikuwa na safari ya kutoka Malaysia kwenda Algeria, ambapo makubaliano kati ya marekani na Thailand yalifanyika na kumpeleka Hamza mpaka nchini marekani, ilikuwa vipi mpaka jamaa kukamatwa? Kuna ajenti wa alijifanya yeye ni underground hacker kwahiyo anataka kununua SPYEYE ndio alikuwa anaweza kuongea na Hamza na alifanikisha kukamatwa kwa hamza.

Panin pia alikamatwa mwaka 2013 katika uwanja wa ndege wa Georgia International Airpot na wote kwa pamoja wakakutwa wapo chini ya polisi.

Baada ya kukamatwa HAMZA baadhi ya watu ambao wanamsapoti wali-hack website ya Air France pamoja na ile ya Virginia University, wakiwa wanashinikiza kuwa Hamza aachiwe huru, na katika mitandao ya kijamii kulikuwa na hashtag kama Freepalestine na ile ya FreeHamzaBendelladj, na vyuo vya nchini algeria wanampongeza na kumsapoti huku wakimchukulia kama shujaa wao.

HAMZA AMENYONGWA?

Picha inayohusiana

Hukumu ilikuwa inaonyesha kuwa Hamza ataenda jela kwa muda wa miaka 15, lakini baadae ukaja uvumi kuwa Hamza kanyongwa, Lakini balozi wa marekani nchini algeria alikanusha madai hayo na kusema kuwa kuna adhabu ya capital kwa kosa kama hilo kutokana na sheria za marekani

No comments:

Post a Comment

Pages