Leo
hii jicho langu limeangazia katika nchi ya Namibia ambapo kuna jumla ya watu
takribani milioni mbili na makabila (ethnic) takribani 13 Herero, Damara,
Nama, San (Bushmen), the Rehoboth Basters, the Coloureds, the Whites, Caprivian, Kavango, Topnaars, Tswana, the Himba and the Owambo.
Location ya Kijiji
Lakini jicho langu limeangaza Zaidi kaskazini mwa
nchi hiyo katika mkoa wa Kunene linapatikana
makabila maarufu sana. Ambayo ni Ovahimba, Tangu Uhuru wa Namibia kabira hili
bado linaendeleza kuishi kwa kupitia tamaduni na mila na kujiweka mbali kabisa
na utamaduni wa kimagharib lakini linashirikiana na watu mbali mbali wa
kimataifa ili kukamilisha miradi mbali mbali kama ujenzi wa Hydroelectric Power,
Huku ikikadiliwa lina watu watapatao elfu hamsini.
Maisha yao (Dini/Mavazi/Shughuli za kijamii)
Kabila hili ambalo lina Imani ya Mungu mmoja na
mungu wao anaitwa Makuru, Lakini pia kabila la Herero linamuabudu mungu huyo.
Lakini kila nyumba ina sehemu maalumu ya kuabudu Mungu huyu anayejulikana kama
Mukuru, ambapo wanakuwa na sehemu maalumu wanachoma moto na mzee wa familia
ndio anaenda kuomba, Lakini kutokana Mukuru kuwa muda mwingi yuko bize na mbali
nao basi wanawatumia wazee wa kijiji hiko kama wawakilishi wa mukuru.
Sehemu wanapoabudu mukuru |
Maisha ya kabila hili wamejikita sana Kwenye Ufugaji
na Kilimo, huku utajiri wa jamii hiyo ikiwa ni Idadi ya mifugo ambayo familia
au mtu anamiliki. Mazao kama Mhindi na Mtrama ndio wanalima saana, Lakini
chakula chao kinatokana na maziwa, asali, mayai ya kuku nyama.
Kazi nyingi katika jamii hiyo zinafanywa na wanawake
kama vile kukamua maziwa, kutafuta kuni,kupika, kulisha mifugo nk, Huku kazi
kubwa ya wanaume ikiwa ni kuwinda na kukusanya mawindo hayo hali hii inawafanya
wanaume wawe wanatoka kwenda msafa marefu kutafuta wanyama wa kuwinda.
Mara nyingi kabila hilo asubuhi linakunywa Uji na Jioni linakula Ugali ambao unatengenezwa kwa kupitia Unga wa mahindi au mtama (unajulikana kama Mahungu), Ila katika siku ya ndoa au sherehe ndio wanakula nyama lakini sio kawaida kula nyama
Mara nyingi kabila hilo asubuhi linakunywa Uji na Jioni linakula Ugali ambao unatengenezwa kwa kupitia Unga wa mahindi au mtama (unajulikana kama Mahungu), Ila katika siku ya ndoa au sherehe ndio wanakula nyama lakini sio kawaida kula nyama
Mama akiandaa Chakula |
Nguo zao ni zile ambazo zinatokana na ngozi ya
wanyama, lakini kuna wengine wanavaa ambazo zimetoka viwandani, huku wakiwa
wanavaa viatu ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia matairi ya gari, Lakini
wanawake wa maeneo hayo wanavaa Otjize (mchanganyiko wa fat inayotokana na
maziwa ya ng’ombe pamoja na Ochre), ambayo hii inawafanya kumudu hali ya kukaa
muda mrefu kwa kukosa maji na pia kupambana na hali ya hewa ya Joto katika
maeneo hayo, lakini pia hii inawazuia kuumwa na insect, Hakika wadada wa kabila
hilo ngozi zao muda wote ni nyekundu ikiwakirisha Damu na Dunia, Wanawake
hawaogi ila wanajifukiza na moshi tu.
Mwanamama wa Kabila hilo akiwa anavuta moshi kama njia ya kuoga |
Jamii hii pia ndoa za mitala ndio zinaongoza mtu
mmoja anaoa wake wastani ni wawili, na pili kuna arranged marriage ambapo
watoto wanachaguliwa wachumba wakifika ukubwani wanaoana. Mara nyingi mabinti
wa kabila hilo wamekuwa wakichaguliwa wachumba na baba wao kwa ajili ya ndoa.
Hili kijana wakiume ajulikane kuwa amekuwa Mwanaume ni mpaka pale atapofanyiwa
tohara lakini, kwa motto wa kike anatambulika kama mwanamke mpaka akizaa.
Okujepisa Omukazendu Treatment katika jamii Hiyo
Jamii hii kama mtu utatembelewa na mgeni basi hakika
ni furaha mno kumuona mgeni wake na baadae usiku, Mume anamuacha mke wake alale
na mgeni huku yeye akienda kulala katika Chumba kingine na kama hakuna basi
ataondoka ili kuwaacha. Kitendo hiko ndio kinajulikana kama Okujepisa Omukazendu.
Sababu kubwa ya kufanya hizi kwamba inapunguza Wivu
na inafanya kuwa na Mahusiano mazuri katika Jamii yao, Katika jamii hii hakika
mwanamke hana mawazo yoyote yale ambayo anachangia kwenye maamuzi. Mwanamke
anaweza kukataa kulala na mgeni lakini lazima walale nae Chumba kimoja na mgeni
huyo, Hali hoo pia ipo hivyo hivyo endapo rafiki wa kike wa mke anapokuwa
anamtembelea mwenzake basi ataachwa kufanya nae mapenzi, Japokuwa hii inatokea
mara chache sana.
No comments:
Post a Comment