Albert Einstein: Kutoka kuwa kilaza darasani hadi kuwa nguli wa fizikia - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Sunday, May 20, 2018

Albert Einstein: Kutoka kuwa kilaza darasani hadi kuwa nguli wa fizikia

 Image result for albert einstein

ALBERT Einstein ni mwanasayansi maarufu aliyeleta mapinduzi katika ulimwengu wa sayansi ambapo enzi za utoto wake walimu walimwita kilaza darasani.

Maisha ya awali ya Eistern hayakukubalika kwa walimu kutokana kutokuwa na akili darasani. Juhudi zake binafsi katika kuamini anachokifanya kilimfanya kuwa ‘genius’ yaani mtu mwenye uwezo wa akili wa kiwango cha juu cha Intelligence Quotients- IQ (160-190).

Msomi huyu ambaye alianza kama mjinga, aligeuza ujinga wake kuwa mwanasayansi mashuhuri na katika historia ya duniani hatoweza kusahaulika.

Mwanafizikia huyu raia wa Marekani mwenye asili ya Ujerumani, alifanya mapinduzi ya sayansi ya fizikia, anajulikana zaidi kwa kugundua sayansi ya mabomu ya nyuklia.

Einstein alizaliwa mwaka 1879, huko Ulm, Ujerumani, alipata elimu ya awali katika mji wa Munich. Alikuwa mwanafunzi mwenye kiwango cha akili kidogo baadhi ya walimu wake walidhani kuwa ni walemavu wa akili (mentally handicapped); kutokana na kushindwa kuzungumza vizuri alipokuwa na umri wa miaka tisa.

Hata hivyo, alivutiwa na masuala ya asili ya ulimwengu. Alikuwa na hisia za ajabu ya kushangaza na aligundua kuwapo kwa nguvu isiyoonekana (Invisible forces) inayoongoza sindano ya dira (campass).

Alipokuwa na umri wa miaka 16 aliweza kufanya mahesabu ya kutatua na kufumbua masuala ya fizikia na uhandisi.

Einstein alimaliza elimu ya sekondari akiwa na miaka 16 na hakupenda kuendelea na masomo, akaamua kuachana nayo na kusoma mwenyewe huku akitafuta njia ya kuingia chuo kikuu.

Mwalimu wake akamfukuza kwa sababu ya mtazamo wake ambao ungeweza kuwaathiri wanafunzi wa darasa lake.

Einstein alijaribu kutuma maombi ya kujisajili na chuo cha Federal Institute of Technology (FIT) huko Zurich nchini Uswisi, lakini ujuzi wake wa masomo yasiyo ya hisabati hakuwa na uwezo nayo hivyo kusababisha kufeli mtihani wa kujiunga na chuo hicho.

Kwa ushauri wa mkuu wa chuo, alienda kujiunga na chuo cha Cantonal huko Aarau, Uswisi na kufanikiwa kupata diploma ambayo ilimwezesha kukubaliwa na chuo cha FIT mwaka 1896 ambapo alishindwa awali.

Akiwa hapo, alitambua uwezo wake mkubwa katika masuala ya fizikia kuliko hisabati.
Einstein alifaulu na kuhitimu katika chuo cha FIT mwaka 1900, lakini kwa sababu ya kutoelewana na mmoja wa profesa wake hakuweza kuendelea masomo kutokana na kukosa msaada wa fedha.
Mwaka 1902, aliajiriwa katika chuo cha Bern akiwa mkaguzi, nchini Uswisi, lakini baada kufikisha umri wa miaka 26 alitimiza vigezo vyote vya kumwezesha kufundisha chuo kikuu. Aliandika utafiti wake wa kwanza kuhusu mapinduzi ya sayansi.

Utafiti huo ulimpa umaarufu Einstein, na vyuo vikuu vikaanza kumgombania kwa huduma zake, mwaka 1909, baada ya kutumika kama mwalimu wa chuo cha Bern aliitwa kufanya kazi akiwa profesa msaidizi wa Chuo Kikuu cha Zurich huko Uswiss. Miaka miwili baadaye alichaguliwa kuwa profesa kamili katika Chuo Kikuu cha Ujerumani huko Prague, nchini Czechoslovakia. Ndani ya mwaka mmoja na nusu akarudi katika chuo cha FIT akiwa profesa kamili.
Hatimaye, mwaka 1913, wanasayansi maarufu wa Max Planck na Walther Nernst walisafiri kwenda Zurich kumshawishi Einstein kukubali kuwa profesa wa Chuo Kikuu cha Berlin huko Ujerumani, pamoja kuwa mwanachama kamili wa Chuo cha Sayansi cha Prussia ambapo alikubali hiyo ofa.

Maisha ya awali ya Eistein hayakukubalika kwa walimu kutokana kutokuwa na akili darasani. Juhudi zake binafsi katika kuamini anachokifanya kilimfanya kuwa ‘genius’ yaani mtu mwenye uwezo wa akili wa kiwango cha juu yaani IQ (Intelligence Quotients-160-190).

Einstein alianza kujulikana katika masuala ya Fizikia na umaarufu wake ulizidi kuongezeka kutokana na tafiti zake kukubalika, hatua ambayo ilizifanya kazi zake kupata sifa kem kem katika ulimwengu wa Fizikia.

Akiwa nchini Ujerumani, kipindi hicho chuki dhidi ya Wayahudi iliongezeka, Einstein alianza kupata mashambulizi kutoka kwa wanasayansi wenzake Philipp Lenard na Johannes Stark ambao walikuwa washindi wa tuzo za Nobel katika masuala ya Fikizia.

Wanafizikia hao walianza kuhusisha nadharia ya Einstein kuwa ‘fizikia ni Kiyahudi.’ (Theory of Relativity) hivyo, mwanasayansi huyu alijiuzulu kutoka Chuo cha Prussia cha Sayansi mwaka wa 1933.

Kwa mara kadhaa, Einstein alikuwa akitembelea Chuo cha California Institute of Technology nchini Marekani, ambapo safari yake ya mwisho mwaka 1933 alipewa nafasi katika Institute for Advanced Studies huku Princeton, huko Massachusetts.

Akiwa nchini Marekani, mwaka 1939 Einstein alikuwa mstari wa mbele katika utengenezaji wa bomu la atomiki, alimuandikia barua aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo, Franklin D. Roosevelt kuelezea kuwa Wajerumani wamepiga hatua katika maendeleo ya sayansi, kwamba Adolf Hitler anaweza kuwa wa kwanza kutengeneza silaha za atomiki.

Image result for albert einstein atomic model

Hii ilichochea jitihada za Marekani kutengeneza bomu la nyuklia. Einstein alishtuka na kusikitishwa kutokana fumbo maarufu la Fikizia E = mc 2 ambalo lilionyesha njia ya kutumia katika kutengeza bomu la nyuklia ambalo lililolitumika kulipua mji wa Hiroshima nchini Japan, mwaka 1945.

Einstein alifariki Aprili mwaka 1955 kwa maradhi ya tumbo. Kabla ya kufariki, aliomba mwili wake uchomwe moto, lakini tukio la kushangaza mtaalamu wa magonjwa ya damu (pathologist), Thomas Harvey aliondoa ubongo wakati mwili wake ukifanyiwa uchunguzi. Harvey alichukua ubongo ili kutafuta siri ya kiwango cha akili yake (genius).
Related image

Baada ya kupata kibali ambacho kilikuwa kinakataliwa kutoka kwa mtoto wa kiume wa Einstein, Harvey baadaye aliukata ubongo wa Einstein vipande vipande na kuupeleka kwa wanasayansi mbalimbali kwa ajili ya uchunguzi. Tafiti kadhaa zimefanyika kuhusiana na ubongo wake tangu miaka ya 1980, lakini matokeo yake yamekuwa yakikataliwa au kutopewa heshima yoyote.

Lakini mwaka 1999, uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha Canada ilichapisha utafiti wenye utata unaodai Einstein alikuwa na ukuta usio wa kawaida katika sehemu ya ubongo uliompa uwezo wa Hisabati.

Wakati Albert Einstein anaendelea kutengeneza fedha nyingi, ingawa alifariki mwaka 1955; mwaka huu jarida la Forbes lilimtaja katika nafasi ya 10 kuwa miongoni mwa watu waliokufa lakini wanaendelea kuzalisha fedha. Einstein mwaka huu pekee amezalisha Dola za Marekani milioni 10 kutokana na jina na sura yake kutumika katika bidhaa, mabango, kompyuta, roboti na mifuko.

No comments:

Post a Comment

Pages