KARIBU KATIKA JAMII YA OVaHiMBa MGENI ANAPEWA MWANAMKE KWA AJILI YA KUFARIJIWA - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Friday, June 22, 2018

KARIBU KATIKA JAMII YA OVaHiMBa MGENI ANAPEWA MWANAMKE KWA AJILI YA KUFARIJIWA




Leo hii jicho langu limeangazia katika nchi ya Namibia ambapo kuna jumla ya watu takribani milioni mbili na makabila (ethnic) takribani  13 Herero,  Damara,  Nama,  San (Bushmen), the Rehoboth Basters, the Coloureds, the Whites,  Caprivian,  Kavango,  Topnaars,  Tswana, the Himba and the Owambo.

Location ya Kijiji

Lakini jicho langu limeangaza Zaidi kaskazini mwa nchi hiyo katika mkoa wa Kunene  linapatikana makabila maarufu sana. Ambayo ni Ovahimba, Tangu Uhuru wa Namibia kabira hili bado linaendeleza kuishi kwa kupitia tamaduni na mila na kujiweka mbali kabisa na utamaduni wa kimagharib lakini linashirikiana na watu mbali mbali wa kimataifa ili kukamilisha miradi mbali mbali kama ujenzi wa Hydroelectric Power, Huku ikikadiliwa lina watu watapatao elfu hamsini.

Maisha yao (Dini/Mavazi/Shughuli za kijamii)


Kabila hili ambalo lina Imani ya Mungu mmoja na mungu wao anaitwa Makuru, Lakini pia kabila la Herero linamuabudu mungu huyo. Lakini kila nyumba ina sehemu maalumu ya kuabudu Mungu huyu anayejulikana kama Mukuru, ambapo wanakuwa na sehemu maalumu wanachoma moto na mzee wa familia ndio anaenda kuomba, Lakini kutokana Mukuru kuwa muda mwingi yuko bize na mbali nao basi wanawatumia wazee wa kijiji hiko kama wawakilishi wa mukuru.

himba village
Sehemu wanapoabudu mukuru

Maisha ya kabila hili wamejikita sana Kwenye Ufugaji na Kilimo, huku utajiri wa jamii hiyo ikiwa ni Idadi ya mifugo ambayo familia au mtu anamiliki. Mazao kama Mhindi na Mtrama ndio wanalima saana, Lakini chakula chao kinatokana na maziwa, asali, mayai ya kuku nyama.

Kazi nyingi katika jamii hiyo zinafanywa na wanawake kama vile kukamua maziwa, kutafuta kuni,kupika, kulisha mifugo nk, Huku kazi kubwa ya wanaume ikiwa ni kuwinda na kukusanya mawindo hayo hali hii inawafanya wanaume wawe wanatoka kwenda msafa marefu kutafuta wanyama wa kuwinda.

Mara nyingi kabila hilo asubuhi linakunywa Uji na Jioni linakula Ugali ambao unatengenezwa kwa kupitia Unga wa mahindi au mtama (unajulikana kama Mahungu), Ila katika siku ya ndoa au sherehe ndio wanakula nyama lakini sio kawaida kula nyama

himba child
Mama akiandaa Chakula
 

Nguo zao ni zile ambazo zinatokana na ngozi ya wanyama, lakini kuna wengine wanavaa ambazo zimetoka viwandani, huku wakiwa wanavaa viatu ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia matairi ya gari, Lakini wanawake wa maeneo hayo wanavaa Otjize (mchanganyiko wa fat inayotokana na maziwa ya ng’ombe pamoja na Ochre), ambayo hii inawafanya kumudu hali ya kukaa muda mrefu kwa kukosa maji na pia kupambana na hali ya hewa ya Joto katika maeneo hayo, lakini pia hii inawazuia kuumwa na insect, Hakika wadada wa kabila hilo ngozi zao muda wote ni nyekundu ikiwakirisha Damu na Dunia, Wanawake hawaogi ila wanajifukiza na moshi tu.

himba smoke bath
Mwanamama wa Kabila hilo akiwa anavuta moshi kama njia ya kuoga

Jamii hii pia ndoa za mitala ndio zinaongoza mtu mmoja anaoa wake wastani ni wawili, na pili kuna arranged marriage ambapo watoto wanachaguliwa wachumba wakifika ukubwani wanaoana. Mara nyingi mabinti wa kabila hilo wamekuwa wakichaguliwa wachumba na baba wao kwa ajili ya ndoa. Hili kijana wakiume ajulikane kuwa amekuwa Mwanaume ni mpaka pale atapofanyiwa tohara lakini, kwa motto wa kike anatambulika kama mwanamke mpaka akizaa.

Okujepisa Omukazendu Treatment katika jamii Hiyo


Jamii hii kama mtu utatembelewa na mgeni basi hakika ni furaha mno kumuona mgeni wake na baadae usiku, Mume anamuacha mke wake alale na mgeni huku yeye akienda kulala katika Chumba kingine na kama hakuna basi ataondoka ili kuwaacha. Kitendo hiko ndio kinajulikana kama Okujepisa Omukazendu.

Sababu kubwa ya kufanya hizi kwamba inapunguza Wivu na inafanya kuwa na Mahusiano mazuri katika Jamii yao, Katika jamii hii hakika mwanamke hana mawazo yoyote yale ambayo anachangia kwenye maamuzi. Mwanamke anaweza kukataa kulala na mgeni lakini lazima walale nae Chumba kimoja na mgeni huyo, Hali hoo pia ipo hivyo hivyo endapo rafiki wa kike wa mke anapokuwa anamtembelea mwenzake basi ataachwa kufanya nae mapenzi, Japokuwa hii inatokea mara chache sana.

No comments:

Post a Comment

Pages