FAHAMU SEHEMU YA INTERNET ILIYOFICHWA (DEEP WEB & DARK WEB) - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Thursday, March 8, 2018

FAHAMU SEHEMU YA INTERNET ILIYOFICHWA (DEEP WEB & DARK WEB)

Tokeo la picha la dark web

Hakika ulimwengu huu una mambo mengi ambayo hatuyafahamu bado, kila siku tunaweza kujifunza jambo jipya hadi mwisho wa maisha yetu.
Intaneti ni kitu ambacho kwa ulimwengu huu wa sasa kila mtu anakitumia kwa njia moja au nyingine. Jambo la kushangaza ni kuwa pamoja na kutumika huku kwa intaneti bado kuna mambo mengi ya kushangaza tusiyoyajua.
Je wajua kuwa ipo sehemu ya mtandao wa intaneti iliyofichwa? Sehemu hii inajulikana kama Deep web na Dark web.
Karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe juu ya sehemu hii ya mtandao wa intaneti iliyofichwa (Deep web na Dark web)

  • Deep web ni nini?
Deep web ni sehemu ya intaneti ambayo haionekani kwenye injini pekuzi kama vile Google na Bing — moja kwa moja injini pekuzi haziwezi kuona sehemu hii kwa sababu imefichwa isionekane.
Deep web siyo kitu kilicho nje ya huu ulimwengu bali ni kitu ambacho umekuwa ukikitumia mara kwa mara — barua pepe yako, benki mtandao, meseji zako za Twitter, LinkedIn n.k Taarifa hizi haziwezi kuonekana kwenye injini pekuzi kwa kuwa zinalindwa kwa nywila (password) au kulipiwa ili kuziona.

“Vitu vyote visivyoweza kupatikana kwenye uso wa juu wa mtandao kwa kutumia injini pekuzi ni sehemu ya Deep web”
Ikizingatiwa kuwa tuna mabilioni ya watumiaji wa mtando wa intaneti duniani, hivyo inaelezwa kuwa kuna mamilioni ya taarifa au data zilizoko kwenye Deep web.

Hata hivyo inaminika kuwa Deep web inaunda sehemu kubwa ya mtandao; Deep web inaweza kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida kama vile Chrome na Firefox.

  • Dark web ni nini?

Dark web siyo sehemu tofauti na intaneti bali ni sehemu ya Deep web ambayo haiwezi kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida.

Kwa nini Dark web haiwezi kuonwa kwa kivinjari cha kawaida? Ikizingatiwa kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web ni haramu, si rahisi wahusika wake kuruhusu mambo haya kuonekana kwenye vivinjari vya kawaida.

  • Je kwenye Dark web kuna shughuli gani?
Tokeo la picha la dark web

Uuzaji wa madawa ya kulevya, Uhalifu wa kila namna (uuzaji wa viungo vya binadamu, ajira za kutisha, ugaidi n.k), Wadukuzi hatari wa kompyuta, Uuzaji wa taarifa na vitu vilivyoibiwa, Picha za unyanyasaji wa kingono hasa watoto, Uuzaji wa silaha.
Mawasiliano ya wanaharakati na waandishi wa habari wanaotaka kuibua maswala mbalimbali. Hutumia njia hii kujificha wasije wakakamatwa na serikali au mahasimu wao. Mtandao wa wikileaks unapokea pia taarifa kupitia Dark web.


  • Je tovuti za Dark web zinaperuziwaje?
Tovuti za Dark web zinaishia na anwani mtandao (domain) zenye .onion, ambazo zinaweza kufunguliwa kwa kutumia kivinjari cha Tor pekee.


  • Tor ni kivinjari (browser) cha namna gani?
Tor ni kivinjari kilichotengenezwa na watu wakujitolea (voluntiers) kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambacho hufanya kazi kwa usiri wa hali ya juu wa kuficha mawasiliano pamoja na watumiaji wake.
Tokeo la picha la dark web

Hivyo mtu anayetembelea tovuti fulani au kufanya chochote kwenye mtandao kwa kutumia kivinjari hiki siyo rahisi kubainika.

Kwa mfano unaweza ukawa unaperuzi mtandao kwa kutumia Tor ukiwa Tanzania lakini ukaonekana mara uko Japan, mara Uingereza au hata Marekani.T browser

Ikumbukwe kuwa kutembelea Dark web siyo kinyume cha sheria lakini kufanya vitu huko kunaweza kuwa kinyume cha sheria kutokana na tovuti nyingi kufanya vitu vinavyokiuka sheria.

Kwenye Dark web siyo mahali panapovutia kama sehemu ya kawaida ya mtandao wa intaneti tulio uzoea. Tovuti nyingi huku zimetengenezwa kwa makusudi maalumu au pengine ya siri, hivyo hazikujali wala kukulinda.

Ili kuperuzi kwenye Dark web ni lazima uwe na kiungo (link) cha tovuti unayotaka kutembelea kinachoishia na .onion kwa mfano http://zqktlwi4fecvo6ri.onion. Hii ndiyo Dark web, hakuna kugoogle hapa; mambo yanaenda kwa namna ya ajabu ajabu tu.

  • Je Dark web ni mbaya?

Hapa kuna majibu mawili ndiyo na hapana. Pamoja na kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web sio halali, bado kuna toleo lake la Facebook na ProPublica kwa anauani ya .onion.

Lakini ukumbuke kuwa wachambuzi wa mambo wanasema tovuti hizi zinaweza zisiwe za kweli, kwani si rahisi Fecebook kukubali watumiaji wake kutumia anwani za kujificha za .onion. Hivyo kuwa makini na taarifa zako za siri huku.

Uzuri wa Dark web ni kuwa inawawezesha waandishi wa habari, wanaharakati na wale wanaoibua taarifa za siri kuwasiliana na kubadilishana taarifa bila wao kujulikana.

Ni wazi kuwa hakuna kitu kibaya kwenye mtandao bali ni matumizi pekee ndiyo hukifanya kiwe kibaya.

  • Neno la mwisho

Naamini umejifunza mengi ambayo hukuwa unayafahamu kuhusu sehemu ya intaneti iliyofichwa. Lakini pamoja na hayo uliyojifunza ningependa kukushauri kuwa makini sana kama utaamua kutumia Dark web. Kumbuka pia kuzingatia sheria kwani uhalifu, maovu na ukatili wa kutisha umejaa kwenye Dark web.

Kwa mfano picha za video za watu wakichinjwa, ubakaji wa watoto, wizi, chuki na ubaguzi husambazwa bila woga wowote. Wadukuzi hatari pia wamejaa kwenye Dark web, hivyo epuka kutoa taarifa zako, kupakua kitu chochote au kufanya muamala wowote. 


ORIGINAL PUBLISHED BY JAMIIFORUMS































No comments:

Post a Comment

Pages