MAISHA YA MOBUTU SESE SEKO KWA UFUPI
Na; Martin Maranja Masese
Joseph-Désiré Mobutu aliyejiita baadaye Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga alizaliwa mnamo 14 Oktoba 1930 Lisala na kufariki mnamo 7 Septemba 1997 huko Rabat, nchini Morocco.. alikuwa Rais na dikteta wa Zaire (Kongo-Kinshasa) kati ya mwaka 1965 na 1997...
Joseph-Désiré Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga Alizaliwa katika Kongo ya Belgiji mwaka 1930.
Akiwa bado kijana baada ya shule alijiunga na "Force Publique" yaani jeshi la kikoloni la Wabelgiji katika nchi ya Kongo. Hadi 1956 akafikia cheo cha staff sajent (staff sergeant) akaacha jeshi na kufanya kazi magazetini kama mwandishi na baadaye uhariri kabla ya kuacha na kuanza kushiriki katika siasa...
Kabla ya kuachana na jeshi, Baada ya uhuru wa Kongo serikali ilimpa cheo cha kanali akawa mkuu wa jeshi la Kongo.
Katika nafasi kama mkuu wa jeshi alishirikiana na Rais wa Kongo wa wakati huo aliyekuwa akiitwa Joseph Kasavubu katika uasi dhidi ya waziri mkuu wa kwanza Patrice Lumumba aliyepinduliwa tarehe 14 Septemba 1960 na kuuawa baadaye...
Mwaka 1965 Mobutu akiwa bado ni kiongozi mkuu wa jeshi la Kongo, aliamua kumpindua Rais Joseph Kasavubu na akachukua uraisi mwenyewe.
Mnamo mwaka 1970 alijirudisha ofisini kwa njia ya uchaguzi uliopangwa naye wenyewe...
Mwaka 1969 alikandamiza upinzani wa wanafunzi wa chuo kikuu kwa nguvi ya kijeshi...
Wanafunzi hao walikuwa wakipinga utawala wake wa kidikteta na pia walikataa utaratibu wa Mobutu kuchukua wanafunzi wengi na kuwapeleka jeshini... hivyo walifanya maandamano katika mji wa Kinsasha na Lubumbashi kushinikiza Joseph-Désiré Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga atoke madarakani..
Zilitokea rapsha na fujo nyingi sana katika maandamano hayo ya wanafunzi wa vyuo vikuu na shule nyingi za sekondari ambayo yalitiwa chachu pia na wananchi ambao walikuwa hawakubaliani na utawala wa Mobutu Sesseko...
Baada ya kuua wanafunzi wengi, Mobutu akiwa anahudumu kama Rais wa serikali ya Kongo, aliamuru wanafunzi 2000 wengine waingie katika jeshi ili wajifunze nidhamu....
Baada ya vurugu zile ambazo zilichukukua maisha ya vijana wengi wa Kongo.., mnamo mwaka 1970/1971 Mobutu alitangaza kile alichoita "Kampeni ya utamaduni wa Kiafrika".
Alibadilisha jina la nchi ya Kongo kuwa Zaire na raia wote waliagizwa kuacha majina yao ya Kikristo yenye asili ya Ulaya na kutumia majina ya asili ya Kiafrika.
Suti za kimagharibi zilipigwa marufuku nchini Zaire na Rais mwenyewe alianza kuvaa suti zilizoiga mfano wa Mao-Tse-Tung, ambaye alikuwa muasisi wa Taifa la kikomunisti la China...
Hapo ndiyo mwanzo wa hata yeye Joseph Desire Mobutu mwenyewe kuanza kujiita "Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga" yaani akiwa ana maanisha "Shujaa mwenye enzi asiyeshindikana".
Katika tasnia ya uchumi, Mobutu akiwa Rais alitaifisha makampuni ya kimataifa yaliyokuwa yakifanya shughuli za kiuchumi nchini Zaire...
Mara nyingi baada ya kuzitaifisha mali za kampuni hizo za madgaribi na ulaya, alikabidhi mali hizo kwa ndugu na wenzake.
alikuwa mjeuri na mtata sana, maana kuna siku alikuwa akisafiri kwenda nje ya nchi aliondoka na wakuu wa majeshi wote pamoja na funguo za maghala yote ya silaha akihofia kupinduliwa na wakuu wake wa majeshi....
Lakini hadi kufikia mwanzoni mwa mwaka 1977 hali ya uchumi nchini Zaire ilianza kwenda mrama.. Uchumi ulizorota kiasi cha kumlazimisha kuwaomba wageni warudi tena... aliamua kuwapigia goti wale aliowafukuza warudi kuwekeza nchini Zaire..
Zipo sababu nyingi, mbalimbali na tofauti za kwanini uchumi wa Zaire uliporomoka sana mwanzoni mwa mwaka 1977,..
Wafadhili wakubwa wa serikali ya Mobutu walikuwa ni Marekani, Ufaransa, Uingereza na Ubelgiji.. waliamua kusitisha huduma zao za ufadhili na misaada baada ya lengo lao la kuidhohofisha dola ya Sovieti kutimia..
Chini ya Mobutu nchi kubwa ya Kongo ambayo yeye Mobutu aliibadili jina na kuiita Zaire ilirudi nyuma kiuchumi..
Mobutu alijitajirisha kupita kiasi wakati nchi yake ilioza kwa rushwa, ufisadi, wizi wa mali za umma, urasimu, utaifishaji na hata kuifanya nchi kuwa kama taasisi ya watu wachache wenye kujiamulia namna ya kujipigia pesa na mali za umma..
Mnamo Mwaka 1984 mali yake ya binafsi, mali ya Joseph-Désiré Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga.. (Mali nje ya Kongo ilikadiriwa kuwa dolar za Marekani bilioni 4).. jaribu kutafakari dola bilioni 4 mwaka 1984 ilikuwa na thamani kiasi gani.. Mobutu alikuwa ni moja ya Rais wenye pesa na ukwasi wa kutisha.. Utajiri binafsi..
Mobutu alikuwa na utajiri usio na mfano barani Afrika kipindi hiko.. Huku watoto wake wakisafiri na ndege ya Concorde Kutoka Kinshasa Hadi Paris Ufaransa Kila Siku Kwenda Shuleni...
Hekalu la Mobutu Sesseko huko kijijini kwao Gbadolite ambako alijenga kiwanja cha ndege chenye uwezo wa kutua Concorde ili iwe rahisi kwake kwenda na kurudi shopping Paris!!
Nchi kubwa za Magharibi kama vile Marekani na Ufaransa walimvumulia na kumsaidia kwa sababu alionekana kama mwanasiasa anayesaidia kupambana na ukomunisti na harakati za ukombozi kwa mfano Angola .
Wakati wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti nchi za magharibi hawakuona haja tena kumsaidia Mobuto.
Tangu 1990 alipaswa kukubali vyama vya upinzani hata akijaribu kuendeleza udikteta wake.
Katika miaka ya 1996 na 1997 waasi waliongozwa na Laurent Desiré Kabila (ambaye ni baba mzazi wa Rais wa sasa wa nchi hiyo, Joseph Laurent Kabila) walienea katika mashariki ya Zaire kwa msaada wa nchi jirani Uganda na Rwanda..
Kuanzia 1967 Laurent Kabila, aliungana na kundi dogo la Parti de la Revolution Populaire (PRP) akaongoza jeshi la Forces Armees Populaires (FAP) lililokuwa na makambi nchini Tanzania na Zambia, lakini aliweza pia kutawala eneo dogo katika milima ya Fizi ya mkoa wa Kivu hadi 1977 alipokufuzwa na jeshi la serikali ya Mobutu.
Baadaye Kabila aliishi Uganda na Tanzania hakuonekana tena Kongo.
Hakushiriki katika uasi wa wanachi dhidi ya serikali ya Mobutu na jitihada ya kuongeza demokrasia nchini.
Alirudi 1996 wakati wa uvamizi wa Kongo ya Mashariki ya wana migambo wa Hutu kutoka
Rwanda..
Mabaki ya jeshi la kihutu kutoka Rwanda walikuwa wamekimbilia Kongo 1994 baada ya mauaji ya kizazi ya Rwanda na sasa walishambulia Wabanyamulenge waliokuwa Watutsi wa Kongo.
Serikali ya Rwanda ilitafuta njia ya kumaliza wana migambo hawa kwa sababu walikuwa tishio kwa utaratibu mpya wa kiutawala wa nchi ya Rwanda.
Hapa walikuwa tayari kusaidia kujenga vikosi vya Wakongo waliokuwa tayari kupambana na Wahutu katika Kongo.., Kabila aliunda muungano wa "Alliance des Forces Democratiques pour la Liberation du Congo-Zaire (AFDL)" akapokea silaha na washauri kutoka jeshi la Rwanda.
Katika muda mfupi Kabila aliweza kujipatia sifa kama kiongozi mwenye uwezo wa kushindana na jeshi la Mobutu aliyejua namna ya kufanya maazimio yake hata bila washauri wake Warwanda aliotegemea bado.
Mambo yalivyokuwa yanazidi kuwa magumu kila uchwao, Mobutu aliamua kumkubali mpinzani wake wa muda mrefu sana, Etienne Tshisekedi kama waziri mkuu, wakati wa mapigano makali sana na waasi wa waliokuwa wakiongozwa na Laurent Kabila...
Lakini jeshi la Kabila likaendelea kusogea mbele. Tarehe 16 Mei 1997, wapinzani walitwaa uwanja wa ndege wa Lubumbashi na Mobutu aliyegonjeka (yaani alikuwa mgonjwa wakati vita hiyo ikipamba moto) alikimbia nchi.
Baadaye ilitangazwa kwamba alifariki nje ya nchi huko nchini Morocco, tarehe 7 Septemba 1997.
Laurent Desiré Kabila alikuwa ameshaingia tayari Kinshasa tangu 20 Mei 1997 na kuchukua utawala... wakati huo Mobutu alikuwa amekwisha kusafiri kwa kisingizio kwamba anakwenda nje ya nchi kupata matibabu.., alifanikwa kurejea Zaire wakati mapambani ni makali... baadaye akakimbili Togo ambako aliomba serikali ufaransa imruhusu aingine Paris, alikataliwa...ndiyo akakimbilia Morocco..,
Akaunti zake nyingi za kifedha zilikuwa nchini Uswisi.. na huko alikuwa mara nyingi akisafiri kutoka Morocco kwenda Uswisi kufuata pesa..
Habari zisizo rasmi zinasema kwamba, aliwekewa virusi kwenye mpira wa kiume (kondomu), ambavyo vilikula uume wake wote na baadaye akahamia Morocco ambako alifika na kuwekwa kizuizini na mauti kumkuta huko.. akiwa na miaka 66.. (mauti yalimkuta akiwa na miezi 4 tu katika kizuizi chake huko nchini Morocco)
Alifariki akiwa kwenye hospitali ya kijeshi katika mji mkuu wa Rabbat, nchini Morocco , taarifa ya madaktari ya jumla ikisema kwamba.. alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya muda mrefu pamoja na kansa.
Inasemekana msiba wake ulihudhuriwa na watu wachache sana tofauti na umaarufu wa jina lake..
Kifo cha Joseph-Désiré Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga.., hakikutangazwa na chombo chochote cha habari nchini Zaire maana ilikuwa ni marufuku kuandika au kutangaza au kuonyesha habari zake nchini Zaire..
Shirika la utangazaji la Uingereza (Reuters), lilitoa taarifa kwamba.. Mobutu ambaye alikuwa muumini wa kanisa katoliki atazikwa kwenye makaburi ya wakatoliki ya Rabat nchini Morocco..
Ila baadaye, mmoja kati ya wasemaji wa familia ya Mobutu ambaye (Reuters), walificha jina lake kwa sababu za kiusalama, alisema kabla Mobutu hajafariki, aliomba mwili wake uchomwe moto.. na majivu ya mwili wake yasambazwe kwenye ardhi ya nchi aliyozaliwa na kuiongoza kama mfalme..
Huyo ndiye Joseph-Désiré Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga.. ambaye mambo yake mengi hayajaandikwa katika makala hii.. yako mengi sana...
(Makala hii imeandikwa kwa kutumia kumbukumbu mbalimbali kutoka katika magazeti, majarida, machapisho, vitabu na makala mbalimbali)
Ahsante...
Martin Michael Maranja Masese,
Mwananchi wa kawaida,
+255719715520
Bakari Bakari
Chief Editor
0659767121
No comments:
Post a Comment