NINAVYOAMINI MIMI: UGONJWA WA LIVERPOOL UNAPOENEA ULAYA - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Saturday, May 24, 2014

NINAVYOAMINI MIMI: UGONJWA WA LIVERPOOL UNAPOENEA ULAYA

NA: Bakari Ally
Simu: 0684-000544

Maisha yanaenda kasi sana huu ni msemo wa Edo kumwembe lakini ukija kuchunguza ni kweli maisha yanakimbia kama mshale wa sekunde hususani kwenye soka.
Tokeo la picha la liverpool 2004 corner
Enzi cha mchambuzi wa soka Dr.leaky Abdalah alikuwa kila siku kwenye mechi ya liverpool lazima alalamike kuwa fulu beki wa liverpool hawakai kwenye post(mlingoti wa goli) wakati wa kupiga kona au faulo ndogo liverpool wakiwa chini ya Rafael Benitez walikuwa wanafunga sana mpira ya kona kwa kuwa kwenye post hakuna mtu.

Wakati huo timu nyingi zilikuwa zinawaweka beki namba 2 na 3 kwenye milingoti ilikuwa ni vigumu sana kuwafunga magoli ya vichwa.

Soka la sasa ni tofauti na miaka ya nyuma manchester ya ferguson ilikuwa kila kona unamuona rafael na evra wapo kwenye post au rafael na rvp,Van persie msimu uliopita (2012/13) aliokoa magoli manne akiwa kwenye post.Tofauti na makocha wengi wa sasa wanakaba man-to-man wanasahau kukaba njia za mipira hususani kwenye kona wengi wanakuwa man-to-man lakini wanasahau kuwa kuna beki na kiungo mkabaji ambao wanaweza kupiga kichwa wakiwa wana kimbia na vichwa vingi vinaelekea kwenye far post ambako golikipa hawezi kufikia ndipo tunajua kwa soka la enzi za Ferguson nalo linasaidia.
Tokeo la picha la liverpool 2004 corner
Mechi ya Atletico na Real kama coentrao na carvajal wangekuwa wamesimama kwenye posti basi wangeweza kuokoa si hapo tu bali hata kama Goli ambalo walifungwa Atletico kama kungekuwa na watu kwenye post ina maana wao wengeweza kuokoa maana kipa tayari ulikuwa umempita,pia mechi ya Atletico na Barcelona Godin asingefunga kama kwenye post kungekuwa na mtu,unakumbuka kwenye Copa del Rey goli la Barcelona lisingepatikana kama kungekuwa na mtu kwenye post na pia mechi ya Madrid na Munich magoli ya Ramosi yasingepatikana kama mtu angekuwa kwenye post hizo ni mfano wa mechi ambazo mtu kiurahisi unaweza kukumbuka ndio maana umekuwa mfano kwangu.

Wanasema kabla ya sekunde 5 inapotekea kona kipa lazima uwapange wabeki wako kwenye post za kona na kipa atakuwa yupo kati ya goli na hapo itakuwa ngumu kuruhusu goli.

Makocha wengi wa kisasa wanasema kuwa kama mabeki wawili wakiwekwa kwenye post ina maana wakabaji watakuwa wachache alafu washambuliaji wengi nalo ni tatizo,Je nini bora wapinzani wawe wengi nyinyi mukabe goli au muache goli wazi ili idadi iwe sawa na wapinzani?

FORGIVE ME

No comments:

Post a Comment

Pages