KUMBUKUMBU: Mechi tatu zilizowakutanisha miamba ya Kaskazini Egypt dhidi ya Algeria - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Sunday, February 10, 2019

KUMBUKUMBU: Mechi tatu zilizowakutanisha miamba ya Kaskazini Egypt dhidi ya Algeria

Na: Bakari Bakari Jr
Simu: 0659767121
Image result for egypt vs algeria match at sudan

Mwaka 2009, ambapo ni kwenye hatua za kugombania kufudhu katika michuano ya  kombe la dunia nchini Afrika kusini, Leo nakumbuka mechi tatu ambazo ziliwakutanisha wababe wa Kaskazini mwa Afrika Egypt (Misri) na Algeria, Nchi hizi mbili zenye asili ya kiarabu zinatenganishwa na nchi ya Libya, Nchi hizo zikiwa ni mahasimu wakubwa sana katika mchezo wa mpira wa miguu.

Mfululizo wa mechi tatu ili kuamua nani ataenda kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Afrika kusini ambayo ndio yalikuwa kwa mara ya kwanza yanafanyika katika ardhi ya Afrika, wakati huo mara ya mwisho kwa Algeria kufudhu michuano hiyo ilikuwa 1986 na Misri mwaka 1990. Mechi ya kumbukizi ilikuwa ile ya mwaka 1989 ambapo pia ilikutanisha waarabu hawa, ambapo katika mechi hiyo ya 1989 refa alikuwa raia wa Tunisia ambaye alikuwa anaonekana kuipendelea Misri katika maamuzi, Mchezaji wa Algeria alienda kumpiga shabiki wa Misri, washabiki walileta fujo, Daktari wa misri alipasuliwa jicho na kioo na  Lakhdar Belloumi ambapo tukio hilo lilimuhusisha golikipa Kamel Kadri kuwa amehusika.

Katika mechi ya mtoano mwaka 2009 ziliwakutanisha tena miamba hiyo ya kaskazini mwa afrika na kuleta mechi ambazo zinavutia sana kutokana na upinzani wao.

MECHI YA KWANZA ALGERIA

Image result for egypt vs algeria match at sudan

Mechi ya kwanza ilichezwa katika mji wa Bilda huku Algeria, ambapo iliwalazimu timu ya taifa ya  Misri kwenda Oman kwa ajiri ya kupunguza presha za mashabiki kwahiyo walienda kujifungia huko, Na pia Algeria wakaamua kwenda nchini ufaransa kuweka kambi yao kwa ajiri ya mechi hiyo.

Matukio mengine nje ya uwanja kocha wa Algeria alikuwa analia katika Press conference huku akisema kuwa usalama wa familia yake ni mdogo ikiwa atapoteza mchezo dhidi ya Misri, Pia manajeshi elfu tano waligeuza mji wa Bilda kuwa kambi yao ya kijeshi kwa muda, Lakini pia mechi hiyo ilikuwa inawakataza watoto kuingia japokuwa walikuwa na tiketi.

Ilikuwa siku ya 07 June 2009 katika uwanja wa Mustapha Tchaker Stadium kulikuwa na watazamaji takribani 26,500, huku Bennet Daniel kutoka South Afrika akiwa ndio muamuzi wa kati akisaidiwa na MALEBO Tok, pamoja na Anjthish Rugesh.

Mchezo ulikuwa na kasi ya juu sana huku mpaka kufikia kipindi cha kwanza kinamalizika matokeo ni 0-0, Baadae kipindi cha pili kilianza mnamo dakika ya sitini Algeria walipata goli kupitia Matmour  60' na dakika ya 64 mchezaji Ghezzal aliipatia goli la pili na  Djebbour 77' anafunga goli, Washabiki wa Misri wanainamisha vichwa chini, Lakini shambulizi la Misri dakika ya 86 linawapatia goli kupitia mkongwe Mohamed Aboutrika. kipenga cha mwisho matokeo Algeria 3-1 Misri.

MECHI YA MARUDIANO MISRI

Ilikuwa ngumu kwa kusema Misri atafudhu katika mechi hiyo lakini waandishi wengi wa Misri ilionyesha kuwa na imani na timu yao huku wakisema kuwa wanaenda kufanya maajabu katika mji wa Cairo ambapo ni nyumbani kwa Misri. Matukio kabla ya mchezo mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Misri Dalila Ziada alisema "Muda huu wa kuachana na kuangalia matatizo ya kiuchumi, kisiasa ila waangalie nini timu inatakiwa kufanya.

Mashabiki wa Misri wakiwa wamevamia kwenye balozi ya Algeria

Wadukuzi wa Misri (Hackers) walifanikiwa ku-hack akaunti ya gazeti la Ech-Chorouk El-Youm, Lakini pia na waalgeria walilipa kwa ku-hack website ya Rais wa Misri pamoja na gazeti la Al Ahram, Huku mechi ya mwaka 1989 ikiwa kumbukumbu na ilikuwa inaongelewa na media za nchi zote.

ALGERIA WAFIKA MISRI

Mechi ilikuwa inatakiwa kuchezwa tarehe 13 November lakini Algeria walifika tarehe 12, Lakini gari ya wachezaji wa Algeria walipigwa mawe na walivunja madirisha hotelini na kuwajeruhi wachezaji watatu pamoja na mmoja wa benchi la ufundi.
Lakini taarifa kutoka kwenye magazeti ya Misri kuwa timu hiyo haikuvamia bali wachezaji wa Algeria ndio walivunja vioo vya gari, maana kioo kilikuwa kimevunjwa kutokea ndani na sio nje.
Matukio haya yalipelekea mechi kuahirishwa kutoka tarehe 13 mpaka 14 ya mwezi November 

MECHI CAIRO

Mashabiki takribani 75,000 waliingia katika mchezo huo, Mechi ilianza na dakika ya tatu ya mchezo timu ya taifa misri ilipata goli kupitia Amr Zaki, na mchezo ulisimama kwa dakika kadhaa kwa vurugu, lakini baadae mpaka mapumziko ilikuwa misri 1-0 Algeria.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na ubabe ulizidi kuongezeka, kufanya mchezo huo kusimama, Mpaka dakika ya 90 Misri 1-0 Algeria ndipo refa akaongeza dakika nane, Hapo ndio Abotrika na Moteab walipochafuka na kutawala mpira katika dakika  za nyongeza na dakika ya 90+5 Misri wanapata goli la pili na full time mpira unaisha Misri 2-0 Algeria



Shabiki alipatwa na majeraha

Kutokana na matokeo ya Cairo yalifanya AGGREGATE kuwa 3-3 kwahiyo mechi ikaamuliwa ichezwe tena katika uwanja wa Neutral(Hakuna mwenyeji) na ndipo kila timu ikaambiwa itaje nchi gani wanataka kucheza mechi ya marudio, Algeria wakachagua Tunisia na Misri wakachagua Sudan,  Bahati nasibu ilichezeshwa na ndipo ikaangukia Sudan.



MECHI YA SUDAN

Katika uwanja wa Al Mareikh katika mji wa Omdurman, Wakati wa timu ya taifa ya Misri inaenda mazoezini, Timu hiyo ilirushiwa mawe, Japokuwa hakuna majeruhi ambae alipatikana. Lakini pia gazeti moja la Misri lilitoa ripoti ya kuwa Washabiki wao walivamiwa na gari kuharibika jambo ambalo lililazimu wapewe escort na polisi wa Sudan.

Pia katika mechi hiyo kila timu ilipewa idadi ya tiketi 9,000 kwa ajili ya mashabiki wake. alafu uwanja ulikuwa na uwezo wa kuchukua watu 41,000 lakini walitakiwa kuuza tiketi za watu 36,000 tu.

Mazingira Kabla ya Mechi huko Sudan waliita polisi 15,000 kwa ajili ya kuweka ulinzi mitaani na uwanjani, Lakini pia ofisi nyingi za serikali pamoja na shule zilifungwa mapema ili kujisha mechi hiyo na kuweka hali ya usalama

Kuanza kwa mechi yenyewe

Kabla ya mechi kuanza kuna shabiki wa Algeria aliingia Uwanjani na kuanza kushangilia

https://i.guim.co.uk/img/static/sys-images/Guardian/Pix/pictures/2009/11/18/1258552448737/An-Algerian-fan-on-the-fi-001.jpg?width=620&quality=85&auto=format&fit=max&s=17243902f35ec62e05d75a329d496bb2

Kila timu ilikuwa na furaha na kuonyesha ubabe kuwa wao ndio wataibuka kidedea na wakati huo Alaa Mubarak alisema kwa kujisifu kuwa "Wao ni Misri wananyanyua vichwa vyao ili kufika mbali" 

Mechi ilitakiwa kupigwa ndani ya Dakika 90 kwamba hakuna dakika za nyongeza ila kutakuwa na matuta tu, Idadi ya wachezaji wa akiba ni saba kwa kila timu na idadi ya substitution zinazotakiwa kufanyika ni tatu tu.

Misri ambayo ilikuwa inanolewa na mzee Mohammed Shehata  huku Algeria kocha wao ni Raabah Saadane vikosi vyao vilikuwa: 
Misri
Golini kulikuwa na Essam El-Hadary, walinzi Wael Gomaa, Hani Said, Abdel-Zaher El-Saqqa, Ahmed Elmohamady, Ahmed Hassan, Ahmed Fathy, Mohamed Aboutrika, Sayed Moawad, Emad Moteab, Amr Zaki.

Algeria

Fawzi Chaouchi, Madjid Bougherra, Rafik Halliche, Anthar Yahia, Mourad Meghni, Hassan Yebda, Yazid Mansouri, Karim Ziani, Nadir Belhadj, Rafik Saïfi, Abdelkader Ghezz.
Refa alikuw Eddy MAilet alipuliza kipenga kuashiria soka lianze mchezo ulitawaliwa na ubabe ambapo ndani ya dakika moja ya mchezo Nadir Beldaj alipata kadi ya njano, mpaka kufikia dakika ya 26 kadi tatu zilishatolewa. ITAENDELEA


























































































































   





































































No comments:

Post a Comment

Pages