ACHANA NA KAMATI, YA SINGIDA UNITED & AZAM FC STARS IJAYO INAFURAHISHA - ⚽Jumba La Michezo⚽

House of History, Sports & Movies

Breaking

Friday, March 22, 2019

ACHANA NA KAMATI, YA SINGIDA UNITED & AZAM FC STARS IJAYO INAFURAHISHA

Tokeo la picha la tff

NA: Bakari Bakari Jr 
Simu: 0659767121

Kuelekea kwenye mchezo wa kufudhu fainali za mataifa ya afrika maarufu kama AFCON 2019 dhidi ya Uganda machi 24 Shirikisho la soka nchini nimeunda kamati na kupewa jina la “Saidia Stars Ishinde” ili kufanikisha Taifa Stars inafudhu AFCON. Hiyo kamati ndani yake kuna Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul Makonda mwenyekiti wa kamati, Katibu wake ni Engineer Hersi Saidi. Wajumbe wengine wa kamati ni Mohamedi Dewji (Mo),Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Mohamed Nassor, Patrick Kahemele Abdallah Bin Kleb, Tedd Mapunda, Philimon Ntaihaja , Farid Nahid, Faraji Asas, Jerry Muro na Haji Manara.
Mwenyekiti Paul Makonda amesema kuwa wana majukumu makubwa matatu watakayoanza nayo kama kamati ni kuirudisha timu kwa wananchi, kuweka maandalizi mazuri ya timu na uwezeshaji wa timu, huku akisema kuwa anataka kukutana na makundi ya watu mbali mbali ikiwemo Wasanii, viongozi wa dini, wanasiasa, wamiliki wa vyombo vya habari.

Tokeo la picha la Mo dewji

Hii kamati naona sio ya watu wa Soka Zaidi ya kuweka wafanyabiashara wapiga debe wawili pamoja na Mkuu wa mkoa, Maana Mohamedi Dewji ni mfanyabiashara japokuwa ni mpenzi sana wa mchezo wa mpira, Farouk Barhoza ni Tanzania Sisi Nyumbani(TSN), Bin Kleb ni AFROIL, Mohamed Nassor ndio hao wakina Mo Dewji, Engineer Hersi ni msimamizi wa GSM, Faraja na Farid Nahid ni ASAS Lakini pia kwa Haji Manara na Jerry Muro hawa ni wapiga kelele kwenye soka kama wapiga debe wa Terminal Mbagala, Patrick Kahemele alikuwa katibu mkuu Simba akaenda AZAM TV kuchukua nafasi ya Charles Hillary Director of Sports.

Tokeo la picha la taifa stars

Sisemi Taifa Stars itafungwa dhidi ya Uganda, Sina maana hiyo kabisa wandugu, Lakini kwenye ukuaji lazima kuwepo na hatua mpaka pale unapokomaa taifa stars yetu haijakomaa lakini hata tukifudhu tutakosa muendelezo kwenye michuano. Lakini tangu tumefudhu michuano ya CHAN enzi za kocha Mbrazili Marcio Maximo mpaka leo hii michuano gani tena tumeshiriki?, hatuna jibu zaidi ya hii michuano yetu ya Afrika mashariki, zimeundwa kamati ngapi za muda kama hii lakini hazijatupeleka popote pale? Je hatujifunzi chochote kwenye hilo.

Serikali inatakiwa ifanye restructuring ya Soka pamoja na michezo mingine, leo hii Bajeti ya michezo ikisomwa bungeni Dodoma ni chini ya 1% hii inaonyesha jinsi gani hatuipi michezo kipaumbele. Na ndio maana kila siku tunatengeneza kamati utadhania ni Harusi, tena kamati zenyewe hazina tija na za muda mfupi, tunakurupuka. Kama tunataka kamati basi isiwe kamati ya Mechi moja, iundwe kamati ambayo ya muda mrefu yenye watu wa soka ambao hao watasaidia kuinua soka letu na sio kamati kujaza Wafanyabiashara utadhania ni kamati ya Uwekezaji na Biashara.
Serikali ifanye mpango kila kanda ijenge Academy moja hapa Nazungumzia dar es salaam, Kanda ya Kusini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Nyanda ya juu Kusini, Kanda ya Kaskazini na kanda ya kati, ambapo watoto watakusanywa kuanzia miaka 15-23, maana yake tutakuwa na timu ya vijana chini ya miaka 17, chini ya miaka 20 na Chini ya miaka 23. Watoto hawa watakuwa wanaelekezwa, kufundishwa na kushiriki michuano mbali mbali ya soka afrika na duniani, muendelezo wa hawa vijana ndio watakuwa wachezaji wetu wa timu ya taifa, Angalia kikosi cha Mali wachezaji saba wa timu ya taifa ni zao la Vijana ambao walikuwa kwenye AFCON  ya vijana wa chini ya miaka 23.

Lakini kitu kingine cha Umuhimu tusiwashikilie wala kung’ang’ana nao hawa watoto twende Tuwatafutie Academy bora Zaidi Ulaya wakacheze wakakuze uwezo wao, Mfano Ivory Cost wana Academy lakini wakikaa na mtoto wanawatafutia nafasi Ulaya na huu ni utaratibu wa Afrika Magharibu kwa Ujumla wao wanaanza kumjenga kimpira lakini anaenda ukuaji wake na maendeleo ni Ulaya, Leo hii kikosi cha Ivory Coast, Senegal, Nigeria wachezaji wote 23 wa timu ya taifa wanaitwa kutokea Ligi mbali mbali za Ulaya tena zile Top five League, Leo hii Stars ikifika huko kwenye michuano tunaweza shindana nao?

Tokeo la picha la croatia world cup

Mwaka jana tumeshuhudia Croatia wakifika fainali kwenye kombe la dunia hii nchi ambayo imepata Uhuru wake 1991, tambua kuwa Croatia ina idadi ya watu million nne, maisha ya Croatia hayana tofauti na wale wabrazili ama wargentina waliojaliwa na vipaji huku wakicheza soka mitaani, nchi hiyo ina viwanja vitano tu vilivofika viwango vya UEFA's international standard wachezaji wengi sana waliamua kuondoka nchini mwao kutokana na kukosa misingi ya soka na miundo mbinu bora na timu zilikubali kuwauza kwa bei ndogo sana nchi nyingine za Ulaya zenye maendeleo ya mpira, tazama kile kikosi kilikuwa na wachezaji wawili wanaocheza ligi ya ndani ambao ni Dominik Livakovic anaechezea Dinamo Zagreb na Filip Bradaric wa Rijeka hawa wote walicheza chini ya dakika thelathini, wachezaji wengine wakiwa wametawanyika Ulaya. Sita walikuwa wanatoko Ligi ya Seria A Italy, wanne La Liga Spain, watatu wakitoka Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Urusi, Ukraine na Uturuki wakitoa mchezaji mmoja mmoja ambapo kucheza nje ya Croatia kumewapa uzoefu. Croatia ilikuwa na Ivan Rakitic katika nafasi yake ya kiungo huu ni muhimili mkubwa pale Barcelona, pia ilikuwa na Luka Modric muhimili mwingine mkubwa kwenye klabu yake ya Real Madrid, Ivan Perisic wa Inter Milan, Lovren kutoka Liverpool, ilikuwa kazi rahisi kwa Kucheza dhidi ya Messi ambapo Rakitic kila siku anacheza nae mazoezini au kwenye mechi, Modric anakutana na Messi mara mbili kwenye EL Classico, Lovren anakutana na Harry Kane mara mbili kwa msimu kwanini amuogope.

Hii ndio naona Singida United na Azam FC wanaifanyia nchi yetu kwa maslahi mapana ya Soka letu kuamua kuuza nyota wao kwenye nchi zilizopiga hatua kisoka watchezaji kama Farid Musa na Shaban Idi Chillunda huko Hispania, Tiba John anaweza kwenda Czech Republic, Ally Nganzi ameenda Marekani, wakiungana na wakina Mbwana Samatta, Simon Msuva yuko Morroco, Abdi Banda yuko Afrika Kusini kuna mchezaji ana miaka ishirini anaitwa Michael Lema nchini Austria ambaye ilibaki kidogo tu awe mtanzania wa kwanza kucheza ligi ya mabingwa hatua ya awali lakini aliishia kuwa benchi dhidi ya Fernabache, Martin Tangazi yuko nchini Uturuki, Albert Mandari yuko Ukraine na wachezaji wengine wengi barani Afrika, Ulaya, Amerika na mpaka kwenye nchi za kiarabu haoa ni TFF kufanya juhudi za kuwajua wachezaji na kuwafuatilia, muunganiko wa hawa wachezaji hapo baadae basi timu yetu itakuwa bora yenye wachezaji imara kuliko kuwekeza kwenye kamati lazima tuwe na maandalizi ya soka letu.

No comments:

Post a Comment

Pages